BENDI YA TWANGA WAJIPANGA KWENDA KUPAMBA SHEREHE ZA UHURU WA MSUMBIJI

BENDI ya Muziki wa dansi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ inajipanga kwa ajili ya onyesho lake  litakalofanyika Jijini Maputo nchini Msumbuji.Akizungumza na Tanzania Daima  mwishoni mwa wiki Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter alisema kwamba  anawatangazia wadau wa bendi hiyo kutoa sapoti katika kufanikisha safari hiyo ya Msumbiji.

“Tunatarajia kwenda Oktoba,mipango iko oka na tayari wamepata barua ya mwaliko kutoka ubalozi  wa Msumbiji na wenyewe wanajiandaa kwa kuipokea bendi hiyo” alisema Martin. Aliongeza kwa kusema kuwa kabla ya kupiga siku ya kumbukumbu ya uhuru way Msumbuji pia watatumbuiza sanjari na kumbukumbu ya miaka 21 ya  kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza Samora Machel mbaye kifo chake kilisababishwa na ajali ya ndege.

Hayati Samora alifariki dunia  mpakani  mwa nchi yake na nchi ya Afrika Kusini  wakati akitoka kazini  katika  mkutano  wa nchi zilizo mstari wa mbele  wa ukombozi  Kusini kwa Bara la Afrika , huko Lusaka Zambia.Mbali ya Machel pia shujaa  mwingine atakayekumbukwa siku hiyo ni pamoja na hayati Eduardo Mondlane na mashujaa wengine waliochangia katika kuleta uhuru wa  nchi ya Msumbiji.Kadhalika watafanya maonyesho katika miji ya Pemba na  Nampula.

 Wakati huohuo  Martin alisema  hivi sasa bendi ya Twanga inaendelea na ratiba yake kama kawaida ambapo kesho usiku watarindima ndani ya Club Bilicanas ambapo hukamua kila Jumatano na kuanzia sasa kila siku ya Alhamisi watakuwa Club Maisha  iliyopo Oysterbay .

Baada ya kuwapa kisogo Club Sunciro ya  Sinza , Ijumaa watakuwa Santiago Club Mbagala na Jumamosi watakuwa Mango GardenTwanga City’ huku Jumapili mchana watakuwa katika bonanza la wajanja Leaders Club na usiku TCC Chang’ombe.

Post a Comment

0 Comments