
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Abuu Jumaa leo tarehe 25 Februari 2026 amekutana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika mkutano maalumu wa kutoa shukran zake za dhati kwao kwa kumchagua kuwaongoza Jimboni humo.
Mhe.Mbunge Hamoud amesema hayo leo tarehe 25 kwenye mkutano uliofanyika Malandizi Stendi, Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambao umehudhuriwa na viongozi kutoka kata sita za Mlandizi Mjini.
"Baada ya miezi mitatu kupita ya uchaguzi leo nimekuja hapa ili niwashkuru kwa kusimama nami kwenyw uchaguzi na kunichagua kuwa mwakilishi wenu kwa mara nyingine tena nasema mimi siyo mjanja sana bali ni Mwenyeezi Mungu Mungu amepanga iwe hivi" amesema Jumaa.
" Nawashukuru sana kwa kunichagua kuwa Mbunge wenu, Wabunge wawili wa Viti Maalumu Asha Baraka na Hawa Mchafu pamoja na Madiwani 14wa kuchaguliwa na wa Viti Maalumu watano haya ni mafanikio makubwa kwa sababu nikiangalia safu yote ni majembe huvyo tupeane muda" amesisitiza Mhe.Jumaa.
Amesema kuwa anawashukuru pia kwa kumchagua Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan pia amewaomba wana CCM kumpa ushirikiano Mhe.Rais Dkt Samia hasa katika kipindi hiki ambacho anakwenda kumalizia ngwe yake ili aweze kutekeleza mambo mengi makubwa katika nchi yetu" amesema Mhe. Jumaa.
"Tunatakiwa wote kwa pamoja tumsaidie Mhe.Rais Dkt. Samia ili tuweze kuifikia Tanzania yenye mafanikio na kicheko kwa wote" amesema Mhe.Mbunge Jumaa.
Aidha Mh.Jumaa ameanza kwa kukutana na Kata sita ambazo ni Mlandizi ,Mtambani,Kawawa,Mtongani,Janga na Kilangalanga.
Wakati huohuo ametoa ahadi lukuki ikiwa ni pamoja na kujenga maduka makubwa na ya kisasa Shopping Mall,Machinjio, Shule mpya kata ya Janga, atajenga Zahanati Kata ya Kawawa.
Mhe.Jumaa ameongeza kwa kusema kuwa wamekusudia kujenga jengo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akisisitiza kwa kusema kuwa Mungu akimjaalia atajenga kwa fedha zake mwenyewe.
"Baadaye tutapita katika ofisi zote za Kata kuangalia changamoto walizo nazo na tutazitatua .
Akizungumza kuhusu uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 2027 amewasisitiza Viongozi wote ambao wanajiona hawana uwezo wa kuongoza wajiengue mapema na kuatafuta warithi wao ikiwa pamoja na kuwaandaa vijana wenye wito ambao wana uwezona watakaowavusha katika uchaguzi huo ujao.
Katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu Cha Sita cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Vijijini kimeongizwa na Mwenyekiti wake Mkali Kanusu ambaye amesisitiza kuwa mwakani atagombea tena katika nafasi hiyo.
"CCM ni Chama kizurikinatulea kinatuheshimisha pia runadhaminika hivyo tunendelee kukijenga kwa makundi kwa maslahi ya Chama chetu hivyo wote kwa sasa tukubaliane kufanya kazi na kushirikiana kwa pamoja.
Mimi ndiyo mwakilishi wa Mhe.Rais Dkt Samia hivyo hata kama hunipendi hunitaki wewe njoo tuzungumze kwa maslahi ya Chama chetu ili wote kwa pamoja tulete maendeleo.
"Nimedhamiria kupambana kupandisha Mamlaka ya Mji ,na jambo linakwenda vizuri katika ngazi za juu ikiwamo Wilaya na Mkoa.
Endapo tutapandishwa hadhi tutapata faida ya Mji kupangika kisasa ,kupata ongezeko katika ruzuku barabara zitajengwa katika kiwango cha lami ,pia ikumbukwe kuwa 2025-26 tumeongoza kwa nchi nzima kwa kukusanya mapato hili ni jambo la kujivunia ,tutamaliza ujenzi wa soko ,stendi ya mabasi tutajenga hoteli kubwa na ya kisasa maegesho ya magari.
Aidha Mhe.Jumaa amezitaja baadhi ya barabara ambazo ziko katika mpango wa kujengwa katika kiwango cha lami ni Chalinze Gwata, Utete, Rufiji na Makofia Mlandizi Mzenga.

0 Comments