NEW DELHI, INDIA
MWIGIZAJI wa filamu za kihindi, Katrina Kaif amejikuta akimpiga kibao Imran Khan, zaidi ya mara 16 kutokana na kutafuta kipande kizuri cha kuingiza katika filamu.Tukio hilo lilitokea wakati alipokuwa akipiga picha za filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mere Brother Ki Dulhan’ itakayotoka Septemba 9.Mwigizaji huyo alijikuta akishindwa kupiga picha mara moja na kujikuta akipiga zaidi ya mara 16 ili apate iliyo bora.Akielezea tukio hilo Imran alisema “Siku iliyofuata nilipokuwa nimekwenda kutengeneza sehemu nyingine, nilimwambia Katrina kuwa sikuwa na furaha kucheza sehemu ile ya kumpiga kibao. Filamu hiyo ya ‘Mere Brother Ki Dulhan’ imemshirikisha mwimbaji nyota kutoka Pakistani, Ali Zafar.
0 Comments