WAHITIMU WATAKIWA KUWA MFANO WA KUIGWA


Wahitimu wa Shule ya Msingi na awali ya Pius Pre and Primary school wametakiwa  kuendelea kuwa na tabia njema baada ya kupatiwa  malezi mazuri  Shuleni hapo.

Akizungumza  jana katika mahafali yaliyofanyika shuleni  hapo Mwalimu Mkuu Sospeter  Simon Mabanga  amesema Mabanga nendeni  mkawe chachu  ya maendeleo  katika jamii zenu kwani elimu  mlizopewa hapa shuleni  ni hazina  katika familia na taifa kwa ujumla.

Aidha Mabanga ametoa shukrani  kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kwa kuruhususekta binafsi kutoa elimu  hapa nchini.

Wakati huohuo zawadi za fedha zimetolewa kwa waalimu ikiwa ni mikakati ya kuinua taaluma na utoaji motisha kwa waalimu kutokana na namna walivyofaulisha kwenye mitihani yao ya taifa.

Shule hiyo ya Pius Pre and Primary iko Kongowe Jijini Dar es Salaam.


Katika mahafali hayo mgeni rasmi alikuwa  Dkt. Mwamba Ally Jingu ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha  Uhasibu  (IFM) ambaye ametoa pongezi kwa uongozi pamoja wa wafanyakazi wote kwa kuwasiamia vema wanafunzi hao.

Post a Comment

0 Comments