NEW DELHI, INDIA
NYOTA wa kike wa filamu wa Bollywood, Karisma Kapoor amesema kuwa mdogo wake wa kike, Kareena hataolewa mapema.Kauli ya mwigizaji huyo imekuja siku chache kutokana na mdogo wake huyo kuwa na ukaribu na mwigizaji Saif Ali Khan.Mwigizaji huyo alisema kuwa mdogo wake amepanga kuolewa mwishoni mwa mwaka 2012.Aliongeza kuwa “Kareena hawezi kuolewa mapem,a kama inavyofikiriwa,”.
Alisema kuwa taarifa hizo zilizokuwa zikieleza kuwa atafunga ndoa hivi karibuni zitakuwa za kizushi.
Mwigizaji huyo ambaye amefanikiwa kutamba na filamu kama ‘Dil To Pagal Hai’, ‘Biwi No.1’, ‘Raja Hindustani’, ‘Zubeidaa’ na ‘Mere Jeevan Saathi’ amesema kuwa hawana haraka ya kumuoza mdogo wake kwa kuwa mambo yote tayari yameshazungumzwa.
NFRA SONGEA YANUNUA TANI ZAIDI YA 72,000 ZA MAHINDI MKOANI RUVUMA
-
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
WAKALA wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA)Kanda ya Songea mkoani
Ruvuma,imenunua tani zaidi ya 72,000 za mahindi kutoka kwa ...
4 hours ago
0 Comments