CEO’s WARUDI NYUMBANI NGORONGORO.


Na mwandishi wetu, Ngorongoro 


Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali na mashirika ya Umma wametembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kufanyaa utalii wa ndani kuona vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Ngorongoro ambayo ni kivutio bora cha utalii Africa mwaka 2023 na 2025.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo kaimu mwenyekiti wa CEOs Forum ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) Bw. Ephraim Balozi Mafuru amesema pamoja na utalii ziara hiyo imewapa nafasi ya kutumia jukwaa la wakuu wa taasisi kujadili na kuatafakari kwa pamoja namna bora ya kutekeleza dira ya taifa ya maendeleo 2050. 

“Kama viongozi tumeona tuje kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea Ngorongoro ili kuongeza hamasa kwa jamii katika kuchangia kukuza sekta ya utalii, tumepata fursa ya kujadili michango ya taasisi za serikali na binafsi katika kufanikisha Dira ya 2050”. alisema Mafuru.


Ziara hiyo imefanyika mara baada ya kukamilika kwa Kikao Kazi cha CEO Forum 2026, kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), na kuwakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ufanisi wa utendaji, uwajibikaji na mchango wa taasisi za umma katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Meneja uhusiano wa NCAA Hamis Dambaya ameeleza kuwa ujio wa viongozi hao umekuwa ni fursa muhimu ya kuendelea kuitangaza Ngorongoro kama eneo lenye thamani kubwa ya uhifadhi, utalii, historia na elimu huku ikiendelea kuimarisha uelewa wa wadau kuhusu kuendeleza utalii endelevu na kuhakikisha rasilimali zinazopatikana ndani ya eneo la Ngorongoro zinaendelea kutoa manufaa kwa Taifa bila kuathiri thamani yake kwa vizaz vijavyo.

Post a Comment

0 Comments