MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KIGODA CHA KUMBUKUMBU YA MWL NYERERE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kumbukumbu ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachohusika na masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi, kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutangazwa kwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho, Prof. Pius Yanda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kilichozinduliwa leo.

Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Pius Yanda, akiwa ameketi kwenye Kigoda hicho baada ya kutangazwa rasmi wakati wa uzinduzi.

Mkurugenzi na Kiongozi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akiigiza kusafiri na Ngamia wake, wakati akitoa burudani ya kuimba mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Baadhi ya wageni waalikwa na Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua maonyesho ya vitabu vya kumbukumbu nje ya ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kuzinduz Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo mchana. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Post a Comment

0 Comments