MISS MWANZA KUPATIKANA GOLD CREST JUNI 24

Baadi ya warembo waMiss Mwanza 2011 wakiwa katika pozi.

Na Ripota Wetu Mwanza

SHINDANO la kumsaka mrembo atakayeuwakilisha mkoa wa Mwanza katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2011, litafanyika Juni 24 katika hoteli ya Gold Crest jijini hapa.
Mratibu wa shindano hilo , John Dotto alisema jana kuwa tayari warembo 17 wamethibitisha kushiriki katika shindano hilo linalotarajia kuwa na ushindani wa hali ya juu kufuatia kujitokeza kwa washiriki wa aina tofauti,
Warembo hao jana walianza kambi rasmi ya mazoezi katika hoteli hiyo ya Gold Crest, ambako watakuwa wakifanya mazoezi chini ya wakufunzi tofauti
Dotto aliwataja warembo watakaoingia kambini leo baada ya kushinda vigezo vinavyotakiwa kuwa ni Sabrina Hamad, Irine Karugaba, Jesca Innocent, Diana Robert, Ester Lawrence, Joella Lazaro na Judith John.
Vidosho wengine watakaoingia kambini leo ni Elizaberth Richard, Semen Steven, Lucy Lemes, Monica James, Zena Msekwa, Stelah Charles, Neema Edmund, Elizaeth Zakaria, Kisura James na Lydia Joseph.
Warembo hao juzi walikusanyika katika klabu ya Villa Resort jijini hapa, ambako walifanya maandalizi mbalimbali, ikiwemo kusaini fomu za mkataba kuthibitisha kushiriki shindano hilo .
Shindano la Miss Mwanza mwaka huu linaonekana kuwa na mvuto mkubwa na linatarajiwa kuwa na ushindano wa aina yake baada ya kushirikisha warembo wengi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), kilichopo jijini hapa.
Shindano hilo linaandaliwa na Kampuni ya Sisi Enterntaiment, ambapo mbali na hoteli ya Gold Crest, wadhamini wengine ni Kampuni ya Simu za Mkono ya Vodacom na kinywaji cha Reds.
Kampuni zingine zilizojitokeza kudhamini shindano hilo la Miss Mwanza ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), na Fransac General Suppliers, Star TV, Nyanza Bottling, Flasac General Supplies, Foremost Insurance Brokers, Clara Salon & Boutique, EF Outdoor na Syscorp Group of Company.

Post a Comment

0 Comments