Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi waShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Sunday Kayuni watakutana na makocha32 wa klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza.U 23 v NIGERIA OLIMPIKI
Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ambayo Jumamosi (Juni 18 mwakahuu) itacheza ugenini na Nigeria katika mechi ya marudiano ya mchujo kwa ajiliya Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani London, Uingereza itaagwa kesho.
U 23 itaagwa saa 7 mchana kambini F&J Hotel iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam.Mechi dhidi ya Nigeria itachezwa Uwanja wa Samuel Obgemudia ulioko Benin City,ambapo ni kilometa 320 kutoka Jiji la Lagos.
Waamuzi wa mechi hiyo ambao wote wanatoka Senegal ni Ousmane Fall (mwamuzi wakati), Maguette Ndiaye, Cheikh Toure na mwamuzi wa akiba Daouda Gueye. Kamishnani Emmanuel Zombre kutoka Burkina Faso.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
0 Comments