USIKU WA KOPO KUFANYIKA DODOMA



KAMPUNI ya Entertainment Masters Limited magwiji wa burudani nchini, wameandaa usiku maalum mahsusi kwa ajili ya wakaazi wa jiji la Dodoma.
Usiku huu maalum ujulikanao kama usiku wa Kopo itatawaliwa na nderemo, muziki na vinywaji mbali mbali vya kopo. Lengo haswa ni kuwapa wakaazi wa Dodoma ladha ya burudani inayopatikana katika Ukumbi wa maraha wa Maisha iliyopo Dar es Salaam.
Usiku wa Kopo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 28 Mei 2011 katika Ukumbi wa Royal Village na itafanyika kila siku ya jumamosi katika ukumbi huo huo.
Mbali na muziki pia kutakuwepo na burudani mbalimbali ili kukidhi kiu ya burudani ya wakaazi wa Dodoma kama vile kuonyeshwa Laivu fainali za UEFA kati ya timu ya Manchester United na Barcelona.
Pia kwa kutambua ya kwamba wanafunzi wa vyuo mbali mbali wanahitaji burudani, EML itatoa usafiri wa kwenda na kurudi kwenye kila chuo.
Usiku wa Kopo itawakutanisha wanafunzi wa vyuo na kuwapa fursa ya kubadilishana mawazo.
Muziki katika Usiku was Kopo itaporomoshwa na MaDJ toka Club Maisha ya jijini Dar es Salaam. Madj hao mahiri ni DJ Zero, DJ S-Dizo na Hyperman HK.
Mbali na burudani mbalimbali pia kutakuwepo na zawadi kutoka kwa wadhamini mbali mbali.
Penny Mungilwa
Meneja Uhusiano

Post a Comment

0 Comments