Flag this messageMAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA 6 WA KIMATAIFA WA MAWASILIANO ICT

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano huo wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kuvaa miwani ili kuweza kuona picha iliyokuwa ikionyeshwa ukutani kupitia Screen na Projector (Animation Fils) , wakati alipotembelea Banda la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana Mei 25. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Elimu na Mafunzo, Shukuru Kawambwa (kulia) ni Mkurugenzi wa Designmate Animation Films, Colonel Basavaraj. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Picha ya pamoja na baadhi ya watu waliopresent paper zao.

Post a Comment

0 Comments