****************************************************************
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emanuel Nchimbi, kesho anatararajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza maalumu la kusherehekea siku ya waandishi wa habari ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando ‘Mgosi’, maandalizi ya bonanza hilo yanaendelea vema, ambapo Waziri Nchimbi amethibitisha kuwa mgeni katika bonanza hilo lililopangwa kufanyika ufukwe wa Coco.
Mhando alisema katika kunogesha bonanza hilo wameamua kuweka mbio maalumu za mita 100 ambazo zitawahusisha wahariri wakongwe ambapo washindi watajinyakulia medali mbalimbali.
Aliliomba Jukwaa la Wahariri kuhamasisha wahariri wakongwe kujitokeza kushiriki mbio hizo.
Katika bonanza hilo, timu za vyombo mbalimbali vya habari zinatarajiwa kumenyana katika michezo mbalimbali ikiwamo soka, netiboli, kuvuta kamba na wavu.

0 Comments