NITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI:RC NYONGO

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, amesema ataendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili kukuza uwekezaji na uchumi wa Mkoa wa Pwani, huku akisisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana kiuchumi.
Mhe. Nyongo amesema hayo leo, Septemba 8, 2026, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Abubakar Mussa Kunenge, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Amesema Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa maeneo muhimu kwa uwekezaji nchini na kwamba atashirikiana na viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa rafiki kwa wawekezaji.

Mkoa huu ni wa uwekezaji. Nimezunguka maeneo mbalimbali kutafuta wawekezaji, kwa hiyo niwakaribishe kwa kuweka mazingira wezeshi,” amesema Mhe. Nyongo.

NnnnnAmesema Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa maeneo muhimu kwa uwekezaji nchini na kwamba atashirikiana na viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa rafiki kwa wawekezaji.

Mkoa huu ni wa uwekezaji. Nimezunguka maeneo mbalimbali kutafuta wawekezaji, kwa hiyo niwakaribishe kwa kuweka mazingira wezeshi,” amesema Mhe. Nyongo.

Aidha, Mhe. Nyongo ameomba ushirikiano wa jamii katika kuwajenga na kuwawezesha vijana kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yanayolenga kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla.

Amesema atashirikiana na viongozi wa Mkoa katika kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, mifugo, uchumi wa buluu pamoja na sekta nyingine za uzalishaji.

“Ninaamini utendaji wetu wa pamoja utatumika kikamilifu katika kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kutatua changamoto zao mbalimbali, pamoja na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,” amesema RC Nyongo.

Alhaji Abubakar Kunenge ambaye alikua Mkuu wa Mkoa wa Pwani 2021-26 sasa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. 
RC Nyongo akipokea shada la maua  kutoka kwa Afisa Habari  wa Mkoa wa Pwani Nasra Mondwe.
Ameongeza kwa kusema kuwa  viongozi na wananchi kutumia sheria, kanuni na taratibu katika kutatua migogoro ya ardhi, akisisitiza umuhimu wa kutumia busara na haki ili kupata suluhisho la kudumu.
Ameahidi kulisimamia kwa karibu suala hilo kwa lengo la kuhakikisha migogoro ya ardhi inapungua na wananchi wanapata haki na fursa ya kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.

"Nimeteuliwa hapa siyo kuja kutawala nimeletwa kumsaidia Mheshimiwa Rais lakini nimekuja kuungana nanyi kufanya kazi katika kuwatumikia wananchi ,kazi kubwa tuliyonayo ni kuwatumikia wananchi .

Makabidhiano hayo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani yalifanyika kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Alhaji Abubakar Kunenge ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Wakati huohuo RC Nyongo amesema sasa mimi nimeletwa kuja kuungana na nyinyi sababu natambua ninyi ndiyo watendaji wakuu na ninyi ndiyo 'Problem Solver' za watanzania wanaoishi eneo la Pwani na wanaopita na kila mmoja ajitambue kwa hilo na kwamba mabadiliko haya asiwe na wasiwasi wowote ajue kwamba kinachoongezeka ni kama chumvi kidogo kwenye mchuzi.

Katika hafla hiyo wakuu hao wa Mikoa wote kwa pamoja walisaini hati ya makabidhiano ya wakuu wa Mikoa pamoja na makabidhiano ya taarifa na vitendea kazi tendo lililofanyika mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na wafanyakazi Mkoani hapa.

Post a Comment

0 Comments