Hapa akiwa katika hatua za kunawishwa kwanza kabla ya kula. Hawa ni kina mama aambapo huwa wanaalikwa au waakati mwingine hucheza ngoma hii wwakati maalumu je umegundua nini kilichofichwa?Jibu ni kwamba hapa bbwana harusi na wwapapmbe wake kadhaa wamefunikwa wakilishwa chakula maalum 'SOLO' ambalo huliwa mara baaada ya kufunga ndoa hapa huwa kuna kila aina ya vyakula ambapo hutegemea na uwezo wa familia husika wengine huweka aina 40 ya vyakula na vyoote bwana huvila kidoogokidogo lakini ila zamani walikuwa wakila waliooa tu lakini siku hizi kutokana na kuvunja miiko hata vijana wadogo utaona wanaingia katika uvungu huu.Tena wakati wakila utasikia wakiimbiwa nyimbo za kila namna tena zenye kutoa hamasa na kusifia mambo kadha wa kadha mara ooh bwwana anakula solo na manyamanyama, mara utasikia bwana harusi akiimbiwa mega ee mega ee mmegee mkeo huku kina mama hawa ambao huongozwa na SOMO wa bibi harusi wakipandisshwa mizuka na kuzungusha nyonga zao,ukibahatika kushuhudia unapata burudani.Ndoa hii ilifungwa hivi karibuni katika mitaa ya Manzese Jijini Dar es Salaam.
SENSEI FUNDI AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 70 CHAMA CHA
JUNDOKAN KARATE OKINAWA, JAPAN.
-
Riporter Zainabu A.Hamisi,
Mwalimu wa Karate wa Kimataifa mtanzania Sensei Rumadha Fundi
anayetambuliwa na baraza ya Karate duniani ndiye mwafrika ali...
1 hour ago
1 Comments