Watanzania waishio Uingereza Ijumaa iliyopita walishirikiana na bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ kufanikisha harambe ya kuwachangia waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Akielezea Mchakato Mzima Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka mbele ya wageni rasmi Meya wa Halmashauri ya Ilala, Jerry Slaa na Meya wa Halmashauri ya Kinondoni, Yusuf Mwenda alifananua kuwa Timu ya SAIDIA GONGO LA MBOTO UK imetoa misaada katika makundi matatu:
1. Pesa taslim sh milllion moja na nusu
2. Chakula ambacho kitakabidhiwa mapema wiki hii
3. Nguo, viatu, vitabu na vifaa mbalimbali ambavyo vimepakiwa kwenye kontena tayari kwa safari ya kuja Tanzania
Twanga Pepeta ilifanya onyesho maalum Machi 4 mwaka huu katika ukumbi wa Zhong Hua Garden uliopo Mikocheni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam na kupata kiasi cha milion moja zitakazowakilishwa kwa waathirika hao.
Aidha Asha Baraka alisema shughuli hiyo ya uandaaji na ukusanyaji wa michango hiyo kutoka Uingereza iliandaliwa na Shilla Frisch, Jestina George kutoka MISSJESTINAGEORGE.BLOGSPOT.COM, Frank Eyembe na Baraka Baraka wa URBAN PULSE CREATIVE na Bernard Chisumo kutoka Locus Impex Shipping Co.
Pia Asha Baraka Alitoa shukrani za dhati wa wale wote walioguswa na kuweza kutoa michango yao kwa ajili ya kusaidia wahangwa wa Gongo la Mboto na kuwasihi watanzania wote pale walipo kuendela kutoa michango. Mmoja kati ya wadau wa saidia Gongo la Mboto UK akipakia mzigo wawahanga wa milipuko ya mabomu iliyotokea Februari 16 mwaka huu.
Meya wa Ilala Jerry Slaa akipiga makofi ikiwa ni ishara ya kukubali maneno yaliyosemwa katika hotuba ya Meya wa Kinondoni Yussuph Mwenda katika onyesho la bendi ya Twanga katika onyesho la kuchangiakucha.Kulia ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka.

Post a Comment

0 Comments