Pichani ni Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura, akizungumza na waandishi wa habari leo.
Na Ripota Wetu
Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Afrika Kati, imewasili juzi, jijini Dar es Salaam tayari kuvaana na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kucheza Fainali za Mataifa Afrika (CAN), uliopangwa kupigwa Machi 26 mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema, msafara wa timu hiyo umewasili nusu na awamu nyingine ya wachezaji na viongozi ilitarajiwa kuwasili jana usiku kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways.
Stars inakabiliwa na kibarua kigumu katika mchezo huo kwa kutakiwa kushinda ili kufufua matumaini ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika zilizopangwa kufanyika Guinea ya Ikweta na Gabon.
Katika hatua nyingine msafara wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka (U-23), unatarajia kuondoka Machi 24 mwaka huu.
WAZIRI KOMBO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA MAGHARIBI
B
-
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amesema kuimarika kwa miundombinu ya Mahakama ni
hatua mu...
3 hours ago
0 Comments