YAJUE MAKOSA 6YANANAYOFANYIKA SIKU YA VALENTINE

NEW YORK, Marekani
IKIWA leo ni sikukuu ya Wapendanao au marufu kama sikukuu ya Valentine.
Sikukuu hii ingawa haitambuliki kama moja ya siku maalum za kiserikali lakini imekuwa ikijipatia umaaufu kila kukicha katika pembe ya dunia ikiwa inasherehekewa kila Februari 14 ya kila mwaka. Lakini inawezekana wengi wa wanaofanya hivyo hawatambui utamaduni huu ulitokea wapi? Kihistoria jina la sherehe hii lilitokanana na jina la mtakatifu wa madhehebu ya Kanisa la Roma aliyekuwa akijulikana kama Valentine au Valentinus.
Mtakatifu huyu aliishi duniani katika karne ya tatu mjini Rome wakati wa utawala wa Claudius II ambaye alikuwa amezuia vijana kutooa kutokana na imani kwamba wale walikuwa wanajeshi imara kuliko wale wenye familia na waliooa.
Kutokana na imani hiyo akaona bora azuie vijana kutooa ili waweze kuwa wanajeshi bora lakini Mtakatifu Valentine, alionekana kutokubaliana na hilo la mtawala Claudius na aliendeleza kufungisha ndoa za siri kwa vijana hao. Baada ya kugundulika amekiuka amri ya mfalme, Claudius alitoa amri ya kukamatwa na kuuawa hivyo sasa ili kumkumbuka ndipo ilianzishwa sikukuu hii.
Lakini pamoja na historia hiyo fupi kumekuwa na makosa ambayo yamegunduliwa kufanyika katika sherehe hii ambayo ni maalumu kwa wapenda nao kuzidisha upendo.
Katika sikukuu hii wanaume hasa wamekuwa wakifanya makosa ambayo wameyaona ya kawaida kwao bila ya kujali yanaathiri mahusiano yao kwa kiasi gani.
Kosa la Kwanza: kutozungumza maneno ya hekima
Hakikisha katika siku hii unazungumza maneno ya busara ikiwa ni pamoja na kumuandikia meseji mpendwa wako za kumfurahisha kwani katika uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa wanawake wengi wanapenda kuzawadiwa kadi na kuandikiwa maneno mazuri ya mapenzi huku wakiwa sambamba na wapendwa wao.
Pili: uchaguzi wa zawadi
Mtaalam wa masuala ya saikolojia ya mapenzi Dk. Terri Orbuch anasema zaidi ya asilimia 75 ya wanawake wamekuwa wakipenda kupewa zaidi. Lakini wanaume wengi wamekuwa wakishindwa kuwanunulia zawadi kutokana na fikra potofu wakidhani zawadi nzuri ni kubwa peke yake ndiyo itaweza kumpatia heshima. Wanafikiria zawadi ni lazima ununue vitu kama magari au vito vya thamani na kumbe wanawake hufurahia zawadi za kaaida kama chocolate, kadi, maua ikiwa ni pamoja na kuambiwa maneno matamu ya kimahaba.
Ni vizuri katika siku hii kwenda dukani na kumnunulia mpendwa wako zawadi za maua mazuri, vitabu vya mahaba, DVD za mapenzi, mishumaa, chocolates na nyingine za aina hiyo.
Tahadhari:
jihadhari kuzembea kutoonyesha tabasamu lako unapokuwa na mpenzi wako kwani haistahili kuwa ‘siliasi’ au watoto wa siku hizi wanasema usionyeshe uso wa mbuzi.
Kwa nini unashauriwa kununua zawadi za kawaida hii inakuwa inamsaidia mpenzi wako hata asiyekuwa na uwezo naye kukununulia kama hiyo kwani wengi wamekuwa na mtindo wa kurudisha zawadi inayofanana na ile uliyomnunulia. Iwapo unajua mwenzi wako hana uwezo halafu wewe unamnunulia vito vya samani utampatia shida kukununulia zawadi ambayo itakwenda sawa na ile uliyo mnunulia.
Tatu: kutokabili maudhi
Inashauriwa kwa wapendanao kuandaana kabla ya siku yenyewe kufika na kuhakikisha mnajihadhari kufanya au kumuonyesha mwenzako mambo ambayo unajua yataleta maudhi kwake hivyo kufanya siku hiyo kuwa mbaya kwenu.
Tahadhari: Unashauriwa ujihadhari kutafuta filamu za kuhuzunisha ambazo zitapelekea kumfanya mwenzi wako apate mawazo hali itakayosababisha kupunguza furaha yenu na kuifanya siku hii kuwa mbaya au kuweka wimbo ambao utaonekana kama kijembe kwake.
Nne: kutochati
Hili la kuchati linasaidia kuongeza upendo kwa wawili na hii haijalishi ni njia gani unaitumia iwe kutuma meseji za simu au barua pepe za mtandaoni au unaweza kutumia mitandao ya Facebook na Twitter hii itamfariji hata yule aliye mbali nawe.
Wakati mwingine unaweza kutumia barua ambayo itakuwa na maneno mazuri ikiwa sambamba na picha ambayo nyuma yake ukiwa umeiandika ujumbe mzuri wa kimahaba ikiwa ni pamoja CD iliyojaa nyimbo za mapenzi ili asikilize ukiwa umempatia kama zawadi.
Tano: kutomsikiliza mwenzio kwa mipango ya familia
Kwa nchini Marekani inadaiwa asilimia 64 za wanafamilia hutumia siku hii kupanga uzazi kwa kusikiliza mipango ya mwenzi wako.
Pia hutumia kuombana misamaha na kuondoa migongano iliyowahi kutokea hapo nyuma.kwani kwa kufanya hivyo siku hiyo itakuwa ya furaha kwa wapenda nao. Kumsikiliza mwenzio kutakuwa kunaonyesha namna unavyomjali mwenzi wako.
Tahadhari:
Kama utakuwa hauna fedha za kumtoa mwenza wako katika sehemu za starehe haimaanishi hata wewe hutasherehekea bali utasherehekea kwa kufurahia na mpenzi wako nyumbani kwako. Unachotakiwa kufanya ni kuandaa chakula ambacho unaamini nyote wawili mnakipenda na kukifurahia huku mkiwa mmewasha mshumaa juu ya meza. Katika meza hiyo unatakiwa kuweka chupa ya kinywaji cha ‘wine’.
Sita: Namna ya uvaaji
Siku hii pia inanamna yake ya kuvaa nia ikiwa kutegena wapenda nao. Kwa mwanamke anashauriwa kuepuka kuvaa jinsi na hii haijalishi ni kwa kiasi gani inakutoa bomba, kwani vazi hili halihamasishi pindi mnapokuwa wawili kwenye mapenzi yenu muda wa jioni.
Pindi unapokuwa na mpenzi wao unatakiwa kuvaa gauni jipya na fupi ambalo litamvutia mwenzio. Kwa upande wa mwanaume anatakiwa avae pamba nyepesi nikimaanisha suluali ya kitambaa na shati la mikono mirefu au mifupi na si vibaya kama utavaa tai ndogo wakati mwingine si vibaya kujipigilia suti.
Imeandaliwa na Shaba Matutu

Post a Comment

0 Comments