SIKUKUU ya Wapendanao ambayo hufanyika kila Februari 14, imeendelea kupata umaarufu kila kukicha.
Sikukuu hii imekuwa ilipata umarufu mjini hapa na duniani kote wananchi wake wamekuwa wakisherehekea siku ya Wapenda nao maarufu kama tofauti na ilivyoanza.
Katika siku hii watu wengi wamekuwa wakiisherehekea kwa kuwasha mishumaa, kununua maua ya mapenzi na kadi kwa kubadilishana baina ya wapenzi zikiwa na jina la Mtakatifu Valentine.
Lakini inawezekana wengi wa wanaofanya hivyo hawatambui utamaduni huu ulitokea wapi na asili yake ni nini, katika makala hii nitazungumzia historia hiyo.
Kihistoria sherehe hiyo ambayo inakadiliwa kuuzwa kadi zaidi kuliko siku nyingine ambako huuzwa kadi zaidi ya milioni 141 kwa nchini Marekani pekee.
Sherehe hiyo imetokana na jina la mtakatifu wa madhehebu ya Kanisa la Roma aliyekuwa akijulikana kama Valentine au Valentinus.
Mtakatifu huyo aliishi duniani katika karne ya tatu mjini Rome wakati wa utawala wa Claudius II.
Katika utawaa wa mfalme huyo alizuia vijana kutooa kutokana akiwa ana amini kwamba wanajeshi imara ni wale ambao wasiokuwa na wanawake.
Kutokana na imani hiyo akaona bora azuie vijana kutofunga ndoa ili waweze kuwa wanajeshi imara na wakakamavu.
Tamko hilo la Claudius lilionekana kumchefua Mtakatifu Valentine ambaye hakutaka kuwaona vijana wakizuiwa kuolewa.
Claudius aliendeleza kufungisha ndoa hizo za siri kwa vijana wa eneo hilo. Siri ya kufungisha ndoa za siri iligundulika kwa mfalme, Claudius alitoa amri ya kukamatwa na kuuliwa.
Historia nyingine zinasema kuwa wakati mtakatifu Valentine alipokuwa jela alianza kumpenda binti wa bwana jela, aliyekuwa akimtembelea kila wakati kabla ya kifo chake alimwandikia barua ya mapenzi na mwisho wa barua hiyo alimaliza kwa kusaini kwa maneno ‘From your Valentine,".
Neno hilo ndipo likapata umaarfu na kuanza kutumiwa hadi leo.
Sherehe hii imepata umaarufu sana nchini Uingereza na Ufaransa.
Kwa nini inasherehekewa Februari 14 kila mwaka? Hiyo ilisababishwa na kifo cha Mtakatifu Valentine aliyekufa mwaka 270 (B.K).
Wengine wanadai kuwa sikukuu hii imelithiwa kutoka kwa wapagani wa zamani ambao walikuwa wakisherehekea ikijulikana kama Tamasha la ‘Lupercalia’.
Sikukuu hii ilihamia na kutambulia rasmi na Papa Gelasius, Februari 14 , 498 baada ya kristo (B.K) ikiwa na maana ya kuhamasisha upendo kwa watu.
Uingereza, Valentine Day ilianza kupata umaarufu katika karne ya 17 hadi 18, ikiwa inasherehekewa kwa marafiki na wapenzi kubadilishana vitufe vidogo na kutumiana ujumbe za kimapenzi.
Hadi mwisho wa karne hizo kulianza kuchapishwa kadi na ile ya kuandika ikapungua na hii ilitokana na mapinduzi ya Teknolojia.
Njia hii ilionekana ni bora zaidi kwani iliweza kufikisha ujumbe moja kwa moja kwa wenza wao kwa kuonyesha hisia zao bila kutumia muda mwingi wa kuandika kwa mkono.
Pia ilishika chati na kupendwa kutokana na uzuri wa lembwa kiasi cha mtu kufikia kuzitunza na kuzithamini.
Nchi ya kwanza kuanza zoezi hilo la kuuza kadi ilikuwa Marekani ambako ilitengenezwa mwanzoni mwa mwaka 1700.
Soko la kadi lilionekana kukuwa kiasi cha kuuza kadi zilizofikia bilioni moja kuuzwa kwa wakati huo wa valentine.
Baada ya mafaniko hayo mwaka uliofuata waliongeza mauzo zaidi kwa kuuza jumla ya kadi zilizofikia bilioni 2.6 kwa mwaka.
Tathmini inaonyesha kuwa kadi nyingi kwa zaidi ya asilimia 85 wanaonunua kadi ni wanawake kwa nchini Marekani.
Sherehe hiyo ya Valentine Day ilipata umaarufu zaidi katika nchi za Canada, Mexico, Uingereza, Ufaransa na Australia.
Na jina la mwanamke wa kwanza kutengeneza kadi za Valentine ilikuwa mwaka 1840 ikitengenezwa na mwanamama, Esther A. Howland.
Mwanamama huyo anajulikana kwa jina la umaarufu la Mama Valentine.
Imeandaliwa na Shabani Matutu kwa msaada wa mashirika ya habari.

0 Comments