Wakati Kocha Mkuu wa Yanga Kostadin Papic akipanga kuondoka nchini Junmatatu ijayo kurudi nchini kwao Serbia , Kocha huyo ametoa msimamo kwa Viongozi wa Yanga kuwa ili aweze kuendelea na timu hiyo apewe nafasi ya kuchagua kocha msaidizi mwingine na si vinginevyo.
Papic, katika mahojiano yetu amekiri kuwa kwanza anaipenda Yanga , ila uongozi wa klabu hiyo haukutenda haki pale ilipomleta kocha msaidizi ambaye Fred Felix Minziro bila ya kumshirikisha kocha huyo kitu ambacho amekitaja ni ukiukwaji wa ueledi wa ukocha.
Lakini P apic anamalizia sakata hili kwa kusema kuwa yupo tayari kufanya kazi na viongozi wa Yanga kwa sharti la kuketi naye tena siku za Jumamosi na Jumapili.
Mbali na menejimenti yenyewe kwa yenyewe kuwa na misimamo tofauti , Klabu ya Yanga ipo katika mgogoro mzito unaotokana na makundi yaliyojigawa ndani kwa ndani kitu ambacho huenda kikatoa mwanya.

Post a Comment

0 Comments