WAZIRI MKUCHIKA:KUANZIA SASA CD UWANJANI 'NO' TUTATUMIA BRASS BAND


Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni , George Mkuchika , ameliangiza shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kuhakikisha kuanzia sasa nyimbo za taifa katika michezo yeyote ya kimataifa zinapigwa na Brass Band, ili kuepuke aibu na fedheha kama zile zilizotokea juzi kwenye uwanja wa taifa wakati wa mechi kati ya Taifa Starsna Morocco.

Akizungumza kwa niamba ya waziri Mkuchika,katibu mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni na Michezo Setti Kamhanda amesema kitendo cha kutopingwa nyimbo za taifa kilichotokea siku ya jumamosi kilisababisha adha kubwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete,mashabiki waliohudhuria mchezo huo na wananchi.

Kamhanda ameongeza kwamba Waziri Mkuchika ameliangiza shirikisho la soka nchini TFF, kuhakikisha linachukua hatua kali dhidi wale wote waliohusika kulitia aibu taifa kwa kushindwa kuwezesha kupingwa nyimbo za taifa wakati wa mchezo kati ya Taifa Stars na Morocco

Wakati Mkuchika akitoa agizi hilo, tayari shirikisho la soka nchini TFF, kupitia kwa Rais wake Leodgar Tengatayai limeshamsimamaisha kazi Afisa habari wake Florian Kaijage kwa uzembe huo na kwamba atisaidia tume itakayoundwa kulichnugza sakata hilo.

Katika mchezo huo wa kundi D, uliochezwa kwenye Uwanja Taifa Jijini Dar es Salaam timu ya Taifa Stars ilifungwa bao moja kwa bila na Morocco.

Post a Comment

0 Comments