TIGO WAZINDUA HUDUMA YA MALIPO KABLA (TIGO PREPAID BLACKBERRY)

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Patrick Makungu leo mchana amezindua rasmi huduma ya malipo kabla ya Blackberry inayotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo (Tigo Pre Paid Blackberry) katika uzinduzi uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinsi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Makungu alisema anayo furaha kubwa na Kampuni ya Tigo iliyozindua huduma kabambe ya malipo ya kabla ya mtandao wa Intanet ya Blackberry kupitia mtandao wa Tigo – Tigo Pre paid Blackberry

Kwa niaba ya Serikali kupitia Wizara Mawasiliano Sayansi na Teknojia kwanza nawapongeza kwa hatua hii kubwa na nzuri mliyofikia ya kuamua kuleta huduma hii ya Blackberry malipo ya kabla ambayo kama mlivyosema mmeitikia ombi toka kwa wateja mnaowahudumia

Pili ninawapongeza kwa kuweka vifurushi vya viwango vya chini zaidi na nafuu kuliko mtandao wowote nchini katika huduma hii ya Blackberry malipo ya kabla. Vifurushi hivyo vinaanzia kiasi cha sh, 7,000, ambapo utapata huduma ya Intaneti kwa juma moja na kuendelea.
Zuri zaidi ni kwamba nyie mmeweka kiwango cha chini kabisa cha kulipia shilingi elfu saba tu kwa siku saba na mteja akafurahia huduma ya intaneti! Hongereni kwa hilo

Hayo yote ni mafanikio na ndiyo maana hata mlitunukiwa ubora wa huduma za mawasiliano nchini na wataalamu wanaofanya utafiti kwenye zaidi ya nchi 80 “Superbrand” hivyo yote hayo ni matunda ya uwekezaji wenu kwa wateja wenu kutokana na bidhaa mnazowapatia

Hivyo sasa kwa niaba ya serikali ninawaomba muendelee kusaidia jamii kwa kuboresha mawasiliano yawe ya kisasa zaidi kwa kuibuka na vitu vipya vingi vitakavyorahisisha mawasiliano na kupitia hilo wananchi waweze kuboresha maisha yao ya kila siku kwa kuwa shughuli zetu za kila siku zinategemea sana mawasiliano

Baada ya kusema haya machache naomba nitamke rasmi kuwa huduma hii ya Tigo Blackberry ya malipo ya kabla imezinduliwa rasmi.
Mwisho.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Sayansi na Teknolojia Dk. Patrick Makungu alikuwa wa kwanza kukabidhiwa zawadi ya simu aina ya Blackberry hapa akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wsa Kampuni Tigo Diego Gutierrezbaada ya hapo ikachezeshwa bahati nasibu kwa wanahabari.
Ofisa Mipango Tigo David Zacharia akielezea huduma hiyo ya mpya yaTigo.
Mkurugenzi wa Tigo Diego Gutierrez hapa akizungumza katika hafla hiyo.
Jimmy kutoka Redio 88.4 Clouds FM akifanya mahojiano na Makungu.
Faraja , Okanda kutoka (Habari Leo na Daily News mwenye kamera) pamoja na Boy Ludovick wakisajili Blackberry zao palepale Kempinski mara baada ya kushinda.
Faraja Kihongole naye aliwakilisha kwa upande wa wanawake alijipatia Blackberry mpyaa akiwa ni kati ya washindi wanne ambao nyota zao ziling'ara.
Boy Ludovick akipokea zawadi yake ya Blackberry mara baada ya kushinda.
Baada ya kushindwa kufurukuta katika bahati nasibu ya Togo Blackberry tukahamia huku kwenye msosi kushoto ni Suleiman Mbuguni (Majira) na mimi. Hapa kulikuwa na pweza, kuku, mbogamboga, viazi mmh acha tuu. Ndani ya Kilimanjaro Kempinski mara baada ya kumaliza kila kitu.
Carren Cyprian kutoka The Guardian Limited.

Post a Comment

0 Comments