Na Juma Kasesa
Mashindano ya kombe la Taifa kwa mchezo wa Netiboli yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kati ya Desemba 12 hadi 18 mwaka huu katika viwanja vya Shule za Filbert Bayi Mkoani Pwani.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania, (CHANETA) Rose Mkisi, alisema, Mikoa yote ya Tanzania Bara inayotarajiwa kushiriki mashindano hayo inatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya Novemba 30 mwaka huu.Alisema licha ya kutakiwa kuthibitisha ushiriki wao mapema, mikoa hiyo itatakiwa kujilipia ada ya ushiriki ambayo ni shilingi 50,000 sambamba na usafiri na chakula huku gharama za malazi zikilipwa na Mkurugenzi wa Shule ya Filbert Bayi.“Mikoa yote inatakiwa kulipia ada na kuthibitisha ushiriki wao mapema ili tupate muda wa kufanya maandalizi kwa ajili ya mashindano,”alisema Mkisi.Aidha Mkisi alisema sababu ya kufanyia mashindano hayo Mkoani Pwani ni kuzipatia mdhamini wa malazi kwa lengo la kuzipunguzia makali timu shiriki.
0 Comments