Jaydee kusherehekea miaka 10 ya muziki


Judith Wambura Lady Jaydee akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 tangu aanze kuimba muziki mwaka 2000 ambapo alikuwa akiimba peke yake (Solo Artist), onyesho hilo litakwenda sambamba na kusherehekea miaka minne ya bendi ya Machozi na kuzindua albamu ya bendi itakayofanyika Agosti 6 mwaka huu katika onyesho litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo katika jengo la Millenium Jijini Dar es Salaam. Kiingilio ni sh.20,000 kwa VIP na siti za kawaida ni sh. 10,000 pia mashabiki watapata Jarida ShearIllusion na CD yenye nyimbo za Lady Jaydee zilizobamba wakati huo hadi sasa.Pia amepanga kuachia albamu yake binafsi hapo mwakani.Kadhalika amesema atawalipia ada watoto wa kike ambao hawana uwezo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne hiyo ikiwa ni katika kuchangia harakati za kumkomboa mtoto wa kike.
Pia kulikuwa na chemsha bongo ya harakaharaka ambapo Jaydee waliwauliza maswali wanahabari walioshinda walipata flana zake zenye nembo ya Jaydee
Hapa akisikiliza swali kutoka kwa wanahabari

Gadna G Habash ambaye ni Meneja wa Jaydee naye alikuwepo

Hapa Jaydee akifafanua jambo

Post a Comment

0 Comments