Diamond sasa ageukia filamu

MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul Juma ‘Diamond’, ametangaza kutengeneza wimbo wake wa ‘Mbagala’, filamu ambayo amesema kwamba itakuwa tayari hivi karibuni.
Diamond amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya kupata filamu hiyo ambayo amesema itakuwa bomba ile mbaya.
Akizungumzia kuhusu kujiingiza katika soko la filamu, Diamond alisema kuwa ni katika harakati zake za kujiongezea kipato zaidi kwa kupitia sanaa.

Post a Comment

0 Comments