FUNDI Sofa, Hamad Witala, mkazi wa Frelimo, mjini hapa amejiua kwa kujinyonga kwa waya wa umeme kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema jana kuwa Witala alijiua wiki iliyopita katika eneo la Frelimo mjini hapa na katika nguo zake kulikutwa barua aliyoiandika akielezea sababu za kujiua.
Katika barua hiyo, kijana huyo alieleza kuwa ameamua kujiya baada ya kumkuta mwanaume ndani ya chumba chake.
Imeelezwa kijana huyo alimkutana mwanaume chini ya uvungu wa kitanda chumbani kwake na baada ya kumuuliza mkewe alidai kuwa ni mteja wa sofa ambaye ameamua kumkaribisha kupumzika chini ya kitanda.
Hata hivyo, kutokana na jazba na jinsi alivyompenda mkewe huyo ambaye alikuwa ametoka kufunga naye ndoa hivi karibuni, aliamua kujinyonga kwa waya wa umeme baada ya mkewe kumuaga anakwenda msibani kwa jirani.
wakati huohuo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Deo Kipinga (24), amekutwa amejiua chumbani kwake. Tukio hilo lilitokea juzi, saa 8.28 mchana katika kijiji cha Kiponzero.
KAMPASI YA TPSC TABORA YATOA MISAADA NA KUFANYA USAFI - KITUO CHA WAZEE
IPULI-TABORA
-
Tarehe 21 Februari 2026,
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania (TPSC), Kampasi ya Tabora imefanya zia...
4 hours ago
0 Comments