NGORONGORO YAZIDI KUVIMBA KIMATAIFA


 Dubai UAE

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kutingisha anga za kimataifa kwa kutwaa *tuzo mbili tofauti kwa mpigo jijini Dubai,Umoja wa Falme za kiarabu zilizotolewa tarehe 28 Novemba 2026.

Tuzo hizo mbili zinahusisha World Public Services Awards imekabidhiwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Ghana Bi  Kokui Hanson na kupokelewa na Meneja wa Uhusiano kwa Umma Hamis Dambaya ikipata tuzo hii kwa kuwa taasisi bora za umma yenye kusimamia uhifadhi na utalii endelevu.

Tuzo ya pili  Ngorongoro  iliyoipokea ni Consumers Choice Awards Africa imepokelewa na Meneja wa Huduma za Utalii na Masoko Kamishna Msaidizi Mwandamizi  Mariam Kobelo,tuzo hii ikiitambua Ngorongoro kuwa taasisi bora katika uhifadhi endelevu na utangazaji na masoko.

Akizungumzia kuhusu tuzo zote hizo mbili SACC Kobelo amesema eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa sasa ni Kama Chanda chema ambapo kila taasisi duniani hutamani kuivika pete.

“Ni ukweli usiopingika kuwa kwa Ngorongoro inafanya vizuri ,tunampongeza Kamishna wa Uhifadhi Dkt.Abdul-Razaq Badru kwa ubunifu na kwa miongozo yake, ni muumini wa mabadiliko chanya na ndiyo maana leo hii kila mdau anaitazama Ngorongoro Kama taasisi bora na ya mfano kuigwa “,amesema bi Kobelo.

Tuzo hizi mbili zinaifanya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Mwaka huu kuzoa tuzo tatu ikitajwa kwamba ni taasisi inayoongoza kwenye uhifadhi,utalii na maendeleo ya jamii duniani.

Post a Comment

0 Comments