Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Nyongo, amewatoa hofu wananchi wa Kijiji cha Fukayosi, Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo, akisisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria wala anayeweza kuinunua Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Nyongo ameyasema hayo Novemba 3, 2026, alipofika kijijini hapo kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima na wafugaji, hususan migogoro inayohusiana na shughuli zao.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga.Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani SACP Salim Morcase akifafanua jambo.
Katika ziara hiyo, amewataka wananchi kuheshimu sheria za nchi na kuacha kujichukulia sheria mkononi. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuundwa kwa mabaraza yatakayoshughulikia migogoro, kuwawajibisha wanaokiuka sheria na kuhakikisha hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wakosaji.
Baadhi ya waananchi waliojitokeza kusikiliza katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika Fukayosi Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani
Vilevile, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika hatua zote za uchunguzi na upelelezi ili watuhumiwa wanaobainika kuhusika na makosa wafikishwe mahakamani na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.











0 Comments