Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa akizungumza wakati wa kutoa mikopo hiyo ya asilimia 10 kwa vikundi 53 yenye thamani ya shilingi milioni 608.9 katika Halmashauri ya wilaya ya Kasulu.
Na Fredy Mgunda, Kasulu
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 608.9 kwa vikundi 53 vya wajasiriamali kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani, unaolenga kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo ya robo ya tatu na ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Hassan Rugwa, alisema mikopo hiyo inalenga kuongeza kipato cha wanufaika, kukuza shughuli za kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Rugwa pia aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi yake, akisema fedha hizo zimekuwa zikielekezwa kwenye shughuli zilizokusudiwa, jambo linaloonyesha uwajibikaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mhe. Charles Kadogo, aliwataka wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanairejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kunufaika.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaack Mwakisu, alisema ameridhishwa na ushirikiano uliopo kati ya ofisi ya wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali, ikiwemo usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, CPA Francis Kafuku, alisema ukusanyaji wa mapato ya ndani unaendelea kuimarika kupitia vyanzo mbalimbali vya kodi, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiari kwani fedha hizo hurejeshwa kwao kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika, Mwenyekiti wa Kikundi cha Tushikamane Mgombe, Anatolia Tinya, alisema kikundi chao kilinufaika na mkopo wa awali, kikaujesha kwa wakati na baadaye kupatiwa mkopo mkubwa zaidi, ambao umewasaidia kupanua biashara, kujenga nyumba na kusomesha watoto hadi elimu ya chuo kikuu.
Katika mgawanyo wa mikopo hiyo, vikundi vya wanawake vilipatiwa shilingi milioni 281.25, vikundi vya vijana shilingi milioni 300.897, huku vikundi vya watu wenye ulemavu vikipokea shilingi milioni 26.817, na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kufikia shilingi milioni 608.9.
KAWAIDA; KASULU DC YATOA MIKOPO YA SHILINGI MILIONI 608.9 KWA VIKUNDI 53 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa akizungumza wakati wa kutoa mikopo hiyo ya asilimia 10 kwa vikundi 53 yenye thamani ya shilingi milioni 608.9 katika Halmashauri ya wilaya ya Kasulu. Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa akionyesha mfano wa hundi ya shilingi milioni 608.9 ambayo imetolewa kwa vikundi 53 katika Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Hizi ni pikipiki zilizotolewa kwa mkopo Na Fredy Mgunda, Kasulu Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 608.9 kwa vikundi 53 vya wajasiriamali kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani, unaolenga kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi. Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo ya robo ya tatu na ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Hassan Rugwa, alisema mikopo hiyo inalenga kuongeza kipato cha wanufaika, kukuza shughuli za kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa. Rugwa pia aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi yake, akisema fedha hizo zimekuwa zikielekezwa kwenye shughuli zilizokusudiwa, jambo linaloonyesha uwajibikaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mhe. Charles Kadogo, aliwataka wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanairejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kunufaika. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaack Mwakisu, alisema ameridhishwa na ushirikiano uliopo kati ya ofisi ya wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali, ikiwemo usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, CPA Francis Kafuku, alisema ukusanyaji wa mapato ya ndani unaendelea kuimarika kupitia vyanzo mbalimbali vya kodi, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiari kwani fedha hizo hurejeshwa kwao kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Akizungumza kwa niaba ya wanufaika, Mwenyekiti wa Kikundi cha Tushikamane Mgombe, Anatolia Tinya, alisema kikundi chao kilinufaika na mkopo wa awali, kikaujesha kwa wakati na baadaye kupatiwa mkopo mkubwa zaidi, ambao umewasaidia kupanua biashara, kujenga nyumba na kusomesha watoto hadi elimu ya chuo kikuu. Katika mgawanyo wa mikopo hiyo, vikundi vya wanawake vilipatiwa shilingi milioni 281.25, vikundi vya vijana shilingi milioni 300.897, huku vikundi vya watu wenye ulemavu vikipokea shilingi milioni 26.817, na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kufikia shilingi milioni 608.9.

0 Comments