Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeendesha mafunzo ya uzingatiaji wa haki za binadamu katika ufikiaji, upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za bahari kwa wavuvi wadogo, vikundi vya kina mama wachakataji wa samaki, TAWFA pamoja na BMU.
Mafunzo hayo yaliyofanyika leo Juni 16, 2026 yamelenga kuelewesha jamii kupitia makundi hayo kuhusu uzingatiaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo, Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume hiyo, Bi. Jovina Mchunguzi ameeleza kuwa mchango wa elimu ya haki za binadamu ni wa wadau wote na si Tume pekee, hivyo wadau wajitokeze kutoa ushirikiano kufikisha elimu.
" Wadau tuungane na Tume katika kufikisha fursa hii kwa wananchi wote, sisi tupo tayari kushirikiana nao " amesema.
"Ninashukuru kupata mafunzo haya, kitu ambacho tulikuwa hatujakipata, tumepata mwamko wa namna gani ya kujihami katika mambo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kujitetea pindi haki zetu zinapozuiliwa" alieleza Mzee Silima Juma, Katibu wa kamati ndogo ya hifadhi kutoka kijiji ch Kiegeani.



0 Comments