Mgeni Rasmi katika ufunguzi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge.
Mashindano hayo yatawakutanisha wanariadha mahiri kutoka Mikoa mbalimbali nchini katika mbio za nyika, yakiwa na lengo la kuibua vipaji, kuhamasisha ushiriki wa michezo na kuimarisha afya pamoja na mshikamano wa Watanzania.
Wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya riadha ya kiwango cha kitaifa.
Kauli Mbiu ya Mashindano hayo "Michezo Huleta Umoja, Amani na Mshikamano kwa Maendeleo ya Taifa letu.

0 Comments