PWANI TUMEJIPANGA KWA AJILI YA UCHAGUZI OKT.29

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge  akizungumza  na Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu kuhimiza wananchi kushiriki  katika Uchaguzi  Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Kibaha, Pwani 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametoa wito kwa wananchi  Mkoani hapa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025.

RC Kunenge amesema hayo leo asubuhi aalipoongea katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo  Ofisini Mkoani hapa.

" Pwani tumejipanga kudhibiti kikundi ama mtu yeyote ambaye atakua na nia ovu ya kuleta vurugu siku ya uchaguzi, wananchi jitokezeni bila ya kuwa na hofu nendeni mkapige kura kisha rudi nyumbani" amesema  Kunenge .

 Natumia nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na mamlaka aliyokuwa nayo ametangaza siku ya kupiga kura kuwa siku ya mapumziko jambo ambalo litaleta utulivu wa watu kwenda kupiga kura.

" Tarehe 29 Oktoba 2025 itakua siku rasmi kwa watanzania kwenda kupiga kura kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani katika mjimbo husika, Serikali tumefanya maandalizi ya kutosha kwa kushirikiana na Viongozi wa dini na mazingira mazuri ya kwenda kupiga kura ambapo kwa Mkoa wa Pwani ina vituo vya kupigia kura 3941 ambavyo vyote vipo jirani na maeneo wanayoishi wananchi.

 " Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejipanga vizuri , natoa onyo kwamba tunazo taarifa za kila eneo ndani ya Mkoa wa Pwani na tunaju nini kitaendelea wananchi nendeni mkatekeleze haki yenu kikatiba" amesema RC Kunenge.

Wakati huohuo ametoa shukrani kwa Waandishi wa Habari ambao wamekua wakifanya kazi kubwa ya kuelelimisha jamii.

Wakaazi wote wa Mkoa wa Pwani shime jitokezeni kushiriki uchaguzi na siku ya uchaguzi ni moja tu amkeni mapema muwahi kwenye vituo vya kupiga kura ambavyo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi jioni utakapofika mwisho wa kupiga kura kila atakayekuwa katika foleni atapiga kura" amema Kunenge.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kuwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ndani ya mkoa yamekamilika Kiulinzi na Usalama huku amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kwenye vituo vya kupiga kura.

Akizungumza leo tarehe 27 Oktoba katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano ofisini kwake amesema kuwa Mkoa wa Pwani una Vituo 3,941 vya kupigia kura vitakuwa wazi kuanzia saa moja asubuhi hadi saa kumi jioni.

"Natoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani wajitokeze siku ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchi nzima kwani hii ni haki yao ya msingi kikatiba wakatimize wajibu wa kuchagua viongozi wao" amesema RC Kunenge.

Akizungumza kuhusu hali ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa amesema kuwa wako timamu hivyo wananchi wasiwe na hofu ya aina yoyote kwani vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejipanga sawasawa katika kuhakikisha hali ya amani na utulivu inaendelea.

Wakati huohuo ametoa onyo kali kwa mtu mmojammoja ama kikundi ambao wataonesha viashiria vya uvunjifu wa amani kwa ni watachukuliwa hatua zinazostahili.


 Wakati huohuo Kunenge ametoa pongezi kwa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Pwani ambao wamekua wakifanya kazi kizalendo

Post a Comment

0 Comments