RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ANAWATAKIA WAISLAMU WOTE MFUNGO MWEMA WA RAMADHANI

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salaam za kuwatakia  Waislamu wote  kheri na mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atuongoze na kutusimamia kwenye Ibada hii muhimu katika imani, aipe kibali cha kheri na kuipokea. 

Katika Ibada hii na kama ambavyo tumeendelea kufanya wakati wote, tuendelee kuitunza na kuiombea nchi yetu amani. Tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kila mmoja kwa nafasi yake kuendelea kutekeleza wajibu wake kwa uadiliu, kwa haki na kweli; na matokeo ya maisha na kazi zetu yawe yenye kumpendeza Yeye, na yenye kulifaa Taifa letu na watu wake. 

Ramadhan Mubarak.

Post a Comment

0 Comments