Akizungumza kuhusu mpango huo, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema wananchi wasio na uwezo, wakiwemo wazee, watoto, wajawazito na watu wenye ulemavu, watagharamiwa na Serikali.
Aidha, amesema kwa gharama ya 150,000, watu sita walio kwenye kaya moja watajiunga na Bima ya Afya kwa Wote itakayojumuisha mwanachama mchangiaji, mwenza wa mwanachama na wategemezi wanne.
“Wategemezi hao wanne wanaweza kuwa ni mzazi wa mwanachama au mzazi wa mwenza wa mwanachama; mtoto wa mwanachama wa kuzaa, kuasili au wa kambo aliye na umri chini ya miaka 21 au ndugu wa damu wa mwanachama aliye na umri wa chini ya miaka ishirini na moja” amefafanua.

0 Comments