WAFANYAKAZI WA OYA WALIOUA MLANDIZI WAFIKISHWA KIZIMBANI

Watuhumiwa wanaokabiliwa na shitaka  la mauaji ya aliyekuwa  mjasiriamali  Juma Said Seif (45) wanaokabiliwa na kesi ya mauaji  namba 
29566  2024 wakiwa wamesimama nje  ya Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani. 
Wafanyakazi wanne wa  Taasisi ya Mikopo almaarufu kwa jina la OYA  leo tarehe 16 Oktoba ,2024 wamefikishwa Mahakamani  kwa kosa la mauaji ya  kukusudia na kumuua Juma Jangalu (45),mkaazi wa Kitongoji cha Mbagala  Mlandizi  Mkoani Pwani katika tukio lililotokea  Oktoba 7,2024 
Akisoma shitaka hilo Wakili wa Serikali Monica Mwela mbele ya Hakimu Mkazi Muandamizi Mfawidhi  wa Mahakama  ya Wilaya ya Kibaha Emmaeli  Lukumai, amesema kuwa kesi hiyo yenye namba 29566 2024 ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza .

Aidha Wakili  wa Serikali Mwela  amewataja watuhumiwa  wa mauaji hayo kuwa ni Dastan John Charles (23)mkaazi wa  Kilangalanga Mlandizi,Abdallah  Felix Wendiliwe (32) mkaazi wa Janga Mlandizi,
Christopher  John Charles (23) mkaazi  wa Kilangalanga na Emmanuel  Joshua Olala(24) mkaazi wa Kilangalanga  Mlandizi Kibaha Vijijini. 
Baada ya kusikiliza shitaka hilo la mauaji,Mhe.
Hakimu Mkazi Muandamizi Mfawidhi wa Mahakama  ya Wilaya  ya Kibaha  Mkoani Pwani Lukumai amesema kuwa  kesi  hiyo ni mauaji ya kukusudia ambayo  imesomwa kwa mara ya kwanza ushahidi bado haujakamilika  hivyo kesi hiyo imeghairishwa hadi  tarehe 30, Oktoba  ,2024 watuhumiwa hawakuruhusiwa 1 kujibu lolote sababu Mahakama  hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Watuhumiwa  wote wamerudishwa rumande kwakua  kosa la mauaji halina dhamana.

Post a Comment

0 Comments