BALOZI NCHIMBI: DEMOKRASIA NA HAKI ZA KIRAIA KUENDELEA KUIMARIKA CHINI YA RAIS SAMIA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza  na  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu , leo tarehe 15 oktoba 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Sera na Tathmini wa Taasisi ya Misaada ya Marekani (MCC), leo tarehe 15 Oktoba 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameithibitishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa masuala ya demokrasia na haki za binadamu yataendelea kuimarika zaidi nchini Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Balozi Nchimbi aliyasema hayo alipokutana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Dr. Mehmet Güllüoğlu, Balozi wa Morocco, Mhe. Zacharia El Goumir, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Sera na Tathmini wa Taasisi ya Misaada ya Marekani (MCC), kwa nyakati tofauti, leo Jumanne, tarehe 15 Oktoba 2024.
Tanzania, huku akieleza dhamira ya Morocco katika kusaidia maendeleo ya kitaaluma na michezo nchini Tanzania.

Aidha, mazungumzo ya Balozi Nchimbi na ujumbe wa MCC, uliongozwa na Mhe. Dan Barnes, yalijikita katika maeneo ya siasa, miradi ya maendeleo na utawala bora.

Balozi Nchimbi alisisitiza kuwa Serikali ya CCM, chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia, inaendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuboresha hali ya demokrasia na haki za binadamu nchini. 

Balozi Nchimbi alisisitiza kuwa maendeleo haya ni sehemu ya dira ya serikali ya kuhakikisha kuwa haki za raia na utawala bora vinadumishwa, huku Tanzania ikiendelea kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na dunia kwa ujumla
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mhe. Zacharia El Goumir , leo tarehe 15 Oktoba 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam

Post a Comment

0 Comments