WAHITIMU JITEGEMEE JKT WAASWA KUTOKUWA NA MAWAZO YA KWENDA NJE YA NCHI

Brigedia Jenerali Petro Ngata  na Mkurugenzi  Mtendaji wa SUMA JKT ambaye pia alikua mgeni rasmi kwenye magafali ya Kidato Cha nne Jitegemee Sekondari akizungumza  na wahitimu  pamoja na wageni waalikwa  hawapo pichani.

Brigedia Jenerali Ngata ameeleza wahitimu hao  kuacha mawazo potofu  ya kwenda nje ya nchi kutafuta maisha badala yake watumie rasilimali za nchi katika  kuongeza pato la Taifa.
Hayo yamesemwa Jijini  Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa (SUMA JKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata wakati wa mahafali ya 40 ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Jitegemee JKT.

Ngata amesema baadhi ya vijana wamekuwa na mawazo ya kwenda nje ya nchi kutafuta maisha mazuri na kuacha rasilimali zilizopo ambazo mataifa ya nje wanazifuata.

"Msitamani kwenda majuu kwani wa huko wanatamani kuja huku kutumia rasilimali zetu ambazo Mungu ametubariki kuwa nazo na hazipo kokote kule zaidi ya Tanzania hivyo tumieni maarifa mliyopata ili kuzitumia,"amesema Ngata
Naye Mkuu wa Shule hiyo Kanali Robert Kesi amesema kuwa wamewaandaa vizuri wanafunzi kwa kufanya mitihani mingi ya majaribio yenye hadhi ya kitaifa kwa nadharia na vitendo na wameiva. 

Awali akisoma risala ya wahitimu Shekha Said amesema kuwa moja ya mafanikio waliyopata ni kujifunza elimu ya ujasirismali ambapo wanaweza kutengeneza sabuni, kilimo cha mbogamboga, kutengeneza balbu zilizoungua na kurudi kufanya kazi kama zamani jumla ya wahitimu 89 wameagwa Shuleni hapo.

Post a Comment

0 Comments