WAZIRI BASHE ATUA JIMBONI KWA MPINA ASISITIZA HATAKI SIASA KWENYE KILIMO

WAZIRI wa Kilimo Mhe. Husein Bashe (Mb) ameta kibabe  jimbo la Kisesa na kukutana na Mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina ana kwa ana.
Aidha Mhe.Bashe ametaka Mbunge huyo kuacha siasa katika zao la Pamba kwani Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inahitaji kuona fedha zinazotengwa zinanufaisha wakulima.
Bashe amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa serikali inarejesha kitalu cha mbegu kuwapatia ruzuku  ya  dawa za wadudu katika zao la mahindi na pembejeo na  mbegu katika zao la Pamba.
Aidha Wazee wa kimila wamemsimika Mhe.Bashe  kuwa Mtemi (Chifu) wa Jimbo hilo.
 
Mpina asema yuko tayari kuweka tofauti zake na Bashe pembeni na kuungana katika masuala ya maendeleo na shughuli za serikali.
Bashe ametua Jimboni humo katika mkutano na wananchi wa jimbo hilo wakati wa kufunga mashindano ya michezo mbalimbali ya Mwandoya na kupokelewa na mamia ya wananchi.
Ametumia fursa hiyo kukutana na Mbunge Mpina ambapo amemtaka kuacha siasa katika zao la Pamba kwa maslahi ya wananchi.
“Rais Samia amefanya kazi kubwa katika kilimo Mpina amesema hapa na mimi nataka nisisitize tuweke mambo mengine pembeni aache siasa na sitaki siasa katika zao la Pamba, nafahamu zipo changamoto lakini tulipotoka siyo tulipo hivyo sitakubali mtu arudishe nyuma jitihada hizi kwani wanaoteseka ni wananchi,”amesema.

Aidha amekabidhi trekta 40 kwa jimbo hilo na kuwataka Maafisa Kilimo na Ugani kuacha kukaa Mijini na kuishi Vijijini ili waweze kuwasaidia wakulima utaalamu na kufikia malengo ya serikali ya kilimo chenye tija.

Bashe amewashukuru wazee wa kimila kwa kumsimika kuwa Mtemi wa jimbo hilo.

“Nami leo nimesimikwa kuwa Mtemi wa Kisesa hivyo Mpina akinitambia pale Bungeni kwa kuingia na fimbo ya Uchifu nami nitaingia na yangu,”amesema Bashe.

Naye Mkuu wa Mkoa huo Kennan Kihongosi amemuhakikishia Waziri Bashe kuwa yeye ndiyo mwenye dhamana na Mkoa huo, hivyo hawezi vumilia watu wanaotafuta umaarufu katika siasa kuingiza masuala ya maendeleo.

“Nimetumwa kazi na Rais Dk. Samia, Simiyu ni ya kwanza ama ya pili katika kuzalisha pamba hivyo kwa wananchi ni zao la kiuchumi sitaki wanasiasa watumie zao hilo kutafuta umaarufu shida zinazosemwa katika zao hilo si za kweli wananchi wa Kisesa msikubali kutumika,”amesema RC Kihongosi. 

Naye Mbunge Mpina ametumia fursa hiyo kumkaribisha Bashe Kisesa na kueleza kuwa wanazo tofauti zao hali iliyowafikisha hadi Mahakamani lakini yupo tayari kushirikiana naye katika masuala ya utendaji wa serikali.

Post a Comment

0 Comments