MAFUNZO KWA MAKOCHA MAAFISA NA ASKARI YAFIKA TAMATI JKT MBWENI

Afisa Mteule Rob Van Belcom  kutoka nchini  Uholanzi alizungumza na wahitimu wa mafunzo hawapo pichani wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa wiki mbili JKT Mbweni.
 13,Septemba,2024.
Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Wakufunzi wa Makocha kutoka nchini Uholanzi ambapo mafunzo hayo yamefungwa jana 13,Septemba, 2024 JKT Mbweni Jijini Dar es Salaam. 
Kutoka Kulia Afisa Mteule Rob Van Belcom  anayefuata ni  Has Feensta  na Sigi Careera a.k.a (Yeba) wakipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika hafla iliyofanyika 13,Septemba,
2024 kwenye Ukumbi wa JKT Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam.13,Septemba 2024.
Afisa Mteule  kutoka  nchini Uholanzi Rob Van Belkom amepokea tuzo maalumu kutoka kwa Brigedia Jenerali  Charles James Ndiege  kwenye hafla  fupi mara baada ya kufunga mafunzo  ya wiki mbili kwa Maafisa na Maaskari yaliyofanyika  JKT Mbweni  Jijini Dar es Salaam 13,Septemba, 2024
Wakufunzi  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo.13,Septemba ,2024 .
 Brigedia Jenerali  Charles James Ndiege  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo 13,Septemba ,2024 hafla iliyofanyika  JKT Mbweni Jijini  Dar es Salaam.
MteuleAfisa Mteule kutoka nchini Uholanzi Rob Van Belkom amepokea tuzo inayoonesha wanyama watano wanaopatikana nchini (Big Five) ikiwa ni katika kumbukumbu kutoka kwa Brigedia Jenerali Charles James Ndiege kwenye hafla fupi mara baada ya kufunga mafunzo ya wiki mbili kwa Maafisa na Askari.


WAKUFUNZI watatu  kutoka nchini Uholanzi  ambao wamekuja kwa ajili ya  mafunzo kwa Makocha 22  kutoka timu za Majeshi  wahitimisha  safari yao.

Akizungumza  kwenye hafla ya kufunga  mafunzo  hayo iliyofanyika Septemba  13 2024  JKT Mbweni Jijini Dar es Salaam Brigedia Jenerali Charles James Ndiege amesema shukran za pekee zimuendee Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jacob Mkunda  kwa  kupitia uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia Conseil International du Sports Military ambao  imewaleta  wakufunzi hao waliowapa ujuzi Makocha ambao ni Maafisa kutoka Jeshi la Ujamiaji na Magereza  walioshiriki mafunzo hayo na Askari kutoka JWTZ. 

"Lengo la  mafunzo haya kwa  Makocha hawa kutoka katika timu zetu za Majeshi nchini  ni    kuwaaendeleza kimichezo na ili uweze kupata mafanikio  yanayoonekana  ni vizuri  ukapata mafunzo,JWTZ tuna timu nyingi  ikiwemo timu ya Mashujaa inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania hivyo haya  mafunzo ni kwa ajili ya kuziendeleza timu zetu" amesema Brigedia Jenerali Ndiege.

"Mafunzo haya yameimarisha mahusiano mazuri  kati ya Tanzania  na nchi ya Uholanzi pia ni matarajio  yetu katika siku za usoni huenda tukabadilishana ujuzi zaidi kwa JWTZ kuchukua  Askari  nchini Uholanzi  hii itategemeana na makubaliano na  CDF Mkunda" amesema Adisa Mteule Rob Van  Belkom. 

Belkom  ameongeza  kwa kusema kuwa anashukuru JWTZ kwa namna walivyo wapa heshima kuba katika kipindi chote cha wiki mbili walizokua nchini na kusifia kupelekwa katika mbuga ya wanyama Mikumi ambapo yeye na wenzake  wameshuhudia kwa macho yao kuona wafalme watano wanyama (Big Five Animal) jambo hili limewafurahisha na kuandika historia katika  maisha yao.

"Tunaahidi kwenda kuwa mabalozi wazuri  wa JWTZ pindi tutakaporudi nchini kwetu" amesema
Belcom.

 Afisa Mteule  kutoka  nchini Uholanzi  Rob Van Belcom mara baada ya  kukabidhi vyeti vya ushiriki wa  wahutimu wa mafunzo hayo kwenye   Ukumbi wa   JKT  Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam .

Baadhi ya Askari waliohitimu mafunzo hayo ya ukocha wa michezo yaliyofanyika JKT Mbweni ni  ni Ashi Hamis Msangula,Anna David Ngati,Sadiki Abdallah, Adam Isack Mollel, Idd Mohammed Salehe,Amran Abdallah Said,Hussein  Uhuru,Mohammed Hussein,Daudi Ramadhan, Emmanuel Joseph Mwijarubi, Francia Kitambala,Athuman Ameir Athuman,Babu Sipendeki Lihundi,Ussi Jeda Haji, Ahmad Abdallah  Mashinga na Irene Raphael Kimaro.
Huku Maofisa kutoka  Jeshi la Uhamiaji ni Yasin Mussa Kisondo na Ofisa kutoka Jeshi la  Magereza  ni Patrick John Lumambo.
Wakati huohuo  kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo bendi  ya  muziki wa dansi ya JKT Mbweni a.k.a Wazee wa Jodari imetumbuiza.

Post a Comment

0 Comments