MHE. SIMBACHAWENE ATETA NA RAIS KIKWETE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete nyumbani kwake Kawe Jijini Dar es Salaam.Septemba 10,2024.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti  na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene leo 10,Septemba ,2024 amemtembelea na kufanya  mazungumzo na  Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete nyumbani  kwake Kawe Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo  hayo Mhe.Simbachawene  amefikisha  Salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan  ambaye ameahidi  kuendelea  kuwa pamoja  na Viongozi  Wakuu Wastaafu wa Kitaifa  kwa maendeleo  ya taifa.
Mhe.Simbachawene amesema Ofisi ya Rais , Menejimenti  ya Utumishi  wa Umma  na Utawala Bora  inajukumu la kutunza  Viongozi  Wakuu Wastaafu Kitaifa na wenza wao,hivyo yuko tayari  kuendelea  kutekeleza jukumu hilo alilopewa na Rais  Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa ufanisi.
Halikadhalika  Mhe.Dkt Kikwete amemshkuru  Mhe.Simbachawene kwa ujio huo  na kupongeza  utaratibu  uliopo wakuwatembelea  Viongozi  Wakuu Wastaafu  wa Kitaifa  kwa kuwa  unawapa faraja,unaonesha thamani na mchango wao kwa maendeleo ya taifa.

Post a Comment

0 Comments