RAIS SAMIA AMEELEKEZA RASILIMALI ZINAZOCHIMBWA NCHINI ZIWANUFAISHE WATANZANIA - DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu  na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amesisitiza ushuru wa Huduma Kutatua 

changamoto 

za  wananchi uchimbaji wa Gesi asili 

kuchochea uchumi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza watanzania kunufaika na rasilimali zinazochimbwa katika maeneo yao kwa kutoa fursa mbalimbali  ikiwemo  ajira.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko  Septemba 10, 2024 Mkoani Mtwara katika hafla ya kukabidhi leseni ya uendelezaji wa eneo la ugunduzi wa gesi asilia katika Kitalu cha Ruvuma, eneo la Ntorya ambapo Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) pamoja na Kampuni za ARA Petroleum Limited na Ndovu Resources Ltd ni wabia.

“ Mhe. Rais alielekeza wananchi waliopo maeneo yenye rasilimali wanufaike kabla ya maeneo mengine, alitoa kibali cha mradi mkubwa wa gesi na tutajenga kiwanda cha kuzalisha gesi na kuboresha kituo za kuzalisha umeme Songa.” 

amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza katika mradi wa Ntorya vitachimbwa visima namba 1 na 2 pamoja na kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka katika kisima hadi Madimba kilomita 34 na katika kipindi cha miezi sita

 bomba litakuwa limejengwa.

Aidha, Dkt. Biteko ameielekeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusimamia utekelezaji wa miradi katika halmashauri kupitia ushuru unaotokana na huduma.

“ Tunakusanya ushuru wa huduma  lakini hatutengi fedha, wakurugenzi wa halmashauri kaeni kwenye mabaraza toeni sehemu ya ushuru wa huduma na kuipeleka kwa wananchi miradi inapofanyika mfano mwaka 2023 TPDC walitoa shilingi milioni 164 na nwaka huu wametoa shilingi milioni 198. Tupeleke fedha kidogo kwa watu kwa kuwa kuna fedha inapatokana kidogo kidogo TAMISEMI  simamieni jambo hili  ili tusipate malalamiko kutoka kwa wananchi, amesema Dkt. Biteko.

Post a Comment

0 Comments