Ununuzi wa Umma (NeST) lililofanyika leo Septemba 9, 2024 jijini Arusha.
Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali zinatambua kwamba fedha nyingi zinazotengwa kwenye bajeti kila mwaka zimekuwa zikitumika kupitia ununuzi wa umma. Kwa kuzingatia hilo, Serikali imekuwa makini kuhakikisha kuwa fedha hizo kupitia ununuzi wa umma zinapata usimamizi makini.
Ambapo kupitia kifungu cha 7 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 ya Mwaka 2023, Serikali imeipa Wizara ya Fedha jukumu la kuhakikisha inaandaa Sera ya Taifa na Mkakati wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ili kuhakikisha ununuzi na shughuli zote zilizofunganishwa katika mnyororo wa ugavi zinazofanyika kwenye taasisi za umma zinazingatia sera hiyo na mikakati itakayowekwa.
“ Naomba Waziri wa Fedha mlisimamie hili na haya ni maelekezo ya Mhe. Rais. Kupitia majukwaa yaliyofanyika yote yametilia mkazo maadili, weledi, uwazi na uwajibikaji na bila maadili wananchi hawezi kupata huduma, pia fedha nyingi zinazotengwa kwa ajili ya wananchi kupata huduma zinaamriwa na kundi hili na kama hatuna taasisi imara za ugavi na ununuzi hatutapata matokeo ya fedha na hatimaye umasikini utaongezeka,” amesema Dkt. Biteko
yaliyofanywa na Serikali kuwa ni kuboresha mfumo wa kisheria na kuweka miundo ya utawala, uboreshaji wa mifumo ya kidijitali, kuajiri na kuwajengea uwezo wafanyakazi, kuboresha upatikanaji wa zabuni kwa Watanzania ambapo ametolea mfano kuwa wazawa wakijengewa uwezo wanaweza kufanyakazi vizuri hata nje ya nchi, pamoja na kuimarisha vita dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
mbalimbali ikiwemo Mfumo wa Uendeshaji Shehena na Mfumo wa Malipo Serikalini (GePG), eGA inasimamia pia Mfumo wa ununuzi wa NeST.
“ Hadi sasa mifumo 164 imeshaunganishwa na kuwezesha kubadilishana taarifa ili kuongeza ufanisi, pia tunahamasisha taasisi zingine zijuinge na mfumo huu ili kuongeza tija ya utendaji.” Amemaliza Mhandisi Ndomba.
Awali Dkt. Biteko amepokea tuzo aliyotunukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha sekta ya ununuzi wa umma nchini. Aidha tuzo ingine imetolewa kwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, Benki ya NMB, Stanbik na TCB, Tanzanine Corporates, Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Suma JKT, BRELA.
Taasisi zingine zilizopewa tuzo ni eGA, Shirika la Mzinga, GPSA, TANESCO na Benki ya Maendeleo ya Kilimo, ISUZU, MSD, Kampuni ya Mtandao wa Simu ya TIGO, Chuo cha Uasibu Arusha, Superdoll, TANROADS, CRDB, NSSF, TRA, Ando, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, TMA, Clouds Media Group, AICC.
Jukwaa hilo la 16 limeongozwa na kauli mbiu inayosema “Utumiaji wa Mifumo ya Kielektroniki kwa Ununuzi wa Umma Endelevu”
0 Comments