Naibu Meya Kinondoni Michael Urio akimjulia hali mgonjwa Ally Kalume
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
NAIBU Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Michael Urio (Diwani ) amemtembelea na kumjulia hali mgonjwa Kalume Ally (41) na kuiomba serikali, viongozi wa Serikali kujitokeza kwa wingi kumsadia matibabu na huduma za kibinadamu.
Mgonjwa huyo Ally Kalume ambaye anasimamiwa kwa ukaribu na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Wa Dar es Salaam (DCPC), amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Kibasila No11,
Awali akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumuona Urio amesema Kalume yupo kwenye maumivu makali na kuuomba u
Uongozi wa Hospitali kumsadia kwa hali na mali.
"Nimefika Wodini, nimebahatika kumuona ndugu yetu, kwa kweli yupo kwenye maumivu makali sana, ameniambia na nimemuona, ombi langu kwa uongozi wa Hospitali ya Muhimbili tumsaidie ndugu yetu huku sisi tukiendelea kuiomba jamiii imsaidie kwa hali na hali, naamini tutafanikiwa" amesema Urio.
Amesema kuwa anaomba Mawaziri, Wabunge, Madiwani na watu mbalimbali kujitokeza kumchagia.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dkt. Rachel Mhavile amesema, mgonjwa huyo alipokelewa Agosti 24 akitokea Hospitali ya Temeke na tayari ameshafanyiwa vipimo vyote.
"Tayari ameshachukuliwa vipimo vyote na tunangoja vipimo tuone tunaanzia wapi, kwa sasa anapewa dawa za kutuliza maumivu , " amesema Dkt. Mhavile kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Mohammed Janabi.
Naye Mwakilishi wa Kamati ya kuratibu matibabu ya Mgonjwa huyo kutoka DCPC, Careen Mgonja, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ukaribu wa Mgonjwa huyo katika kupatiwa matibabu huku akiomba wadau na watu mbalimbali kuendelea kuchangia kupitia namba maalumu ya aliyeteuliwa.
" Watu wote watakaoguswa kusaidia kuchangia mgonjwa wanaweza kutupa kiasi chochote cha pesa kupitia kwa Mratibu Mkuu wa zoezi hili Bi. Kalunde Saidi kupitia namba ya Mtandao wa Airtel
0684695698.
Mgonjwa Ally Kalume Naibu Meya wa Kinondoni Michael Urio na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt.Mhavile.
0 Comments