Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii
Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji
la Tanga Daudi Mayeji wakati alipotembelea kiwanja hicho kabla ya
kuwakabidhi timu ya Coastal Union kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha
Soka mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud kulia ni Mwenyekiti wa timu ya
Coastal Union Steven Mguto
Waziri wa Afya maendeleo ya
Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya
makabidhiano hayo yaliyofanyika Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni
Jijini Tanga
Mkurugenzi
wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed akitoa neno kwenye halfa hiyo
Diwani wa Kata ya Maweni(CCM) Colvas Joseph akizungumza katika halfa hiyo
Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto akizungumza katika halfa hiyo
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga (TRFA) Saidi Soud kushoto akiteta jambo na Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
Mwenyekiti wa baraza la wazee timu ya Coastal Union Salimu Bawaziri akizungumza
Waziri
wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu kushoto
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji katika halfa
hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa TRFA Saidi Soud na Mwenyekiti wa timu ya
Coastal Union Steven Mguto
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa umakini Diwani wa Kata ya Maweni (CCM) Colvas Joseph
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akishiriki kucheza wakati wa halfa hiy |
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu ameipongeza Kampuni ya City Plan kwa kuunga mkono juhudi zao za
kutaka kuimarisha klabu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kwa kuisaidia kupata
kiwanja chao eneo la Maweni Jijini Tanga
Hatua hiyo inatokana na viongozi kufanya kazi kubwa
wakishirikiana na wadau kuhakikisha wanapambana ili kuiwezesha timu hiyo kurudi
kucheza michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kucheza madaraja
ya chini kwa kipindi.
Kiwanja
hicho ambacho kina ukubwa wa square mita 7632 kipo
Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambacho kina gharimu kiasi cha
sh.milioni 38 kimepatikana baada ya kuwepo kwa juhudi kubwa za Waziri
Ummy kuiomba kampuni hiyo kuisaidia timu hiyo eneo lake la kiwanja.
Kukabidhiwa kwa kiwanja hicho inafungua ukurasa mwengine wa mafanikio kwa timu hiyo kongwe hapa
nchini.
Akizungumza leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya kiwanja
hicho, Waziri Ummy alisema kitendo cha kampuni hiyo kutoa eneo hilo kimesaidia
mipango iliyokuwa nayo timu hiyo kuanza kwenda vema huku wakijipanga kwa hatua
nyengine.
Alisema suala hilo linatokana na mshikamano uliopo baina ya
viongozi waliopo wakiwemo wapenzi, mashabiki na wanachama huku wakiwataka
kuuendeleza ili kuweza kupata mafanikio makubwa siku zijazo kwenye michuano ya
ligi kuu.
“Kwanza niwapongeze timu ya Coastal Union kwa kuonyesha
mshikamano na kuweza kupanda daraja kucheza ligi kuu na kama mtu anafanya
vizuri watu wengi wanakuwa tayari kuweza kuwaunga mkono “Alisema.
Alisisitiza kuwa kufanya vizuri kwa timu hiyo kumefanya kuvuta
wadau ambao wameweza kuwasaidia kiwanja nawashukuru kwani wakati tunapongezana
nilihaidi kuwatafutia wadau pia niwaambie bado tunaendelea kutafuta wadau na nihaidi hata ile block yenye square mita
9600 yenye thamani milioni 48 atatafuta wadau ili waweze kupata eneo hilo.
Alisema atasaidia kutafuta wadau ili kupata eneo hilo ambalo
litakuwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa Hosteli,Gym na Ukumbi wa sherehe wa
Coastal Union kwa sababu watu wa Tanga wana fanya sherehe na kitchen party kila
siku .
Hata hivyo alisema pia katika kiwanja ambacho wamekabidhiwa
timu hiyo leo atagharamia gharama za hati za usajili mpaka kupata hati yenye
jina la klabu ya Coastal Union na baadae atakwenda kuwakabidhi
Waziri huyo alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Tanga
wanaotaka kuwekeza waende eneo la Pongwe ambalo lina viwanja 937 hivyo watu
waende kuwekeza kwa sababu Coastal Union wakiwa hapo itavutia lakini pia
ameitaka kampuni hiyo kuwepo kwa eneo kwa ajili ya zahanati kama walivyofanya
kutoa kwa shule ya Msingi
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mayeji alimpongeza Waziri Ummy
kwa kazi kubwa kwa kuongea na wadau kuona Coastal Union inapata sehemu ya
kufanyia mazoezi na mafunzo ya soka kwani jambo hilo linaonyesha namna
alivyokuwa na dhamira kubwa ya kusaidia kuinua michezo mkoani Tanga akiwa namba
moja Sports Lady namba moja.
Kwa hilo Mh Waziri umefanya kazi kubwa sana kwani hatua hiyo
inaisongeza timu ya Coastal Union kwenye mafanikio kutokana na kupata eneo
ambalo wataweza kulitumia kufanya mazoezi na masuala mengine ya kimichezo “Alisema
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto
alisema furaha kubwa aliyonayo huku akiimshukuru Waziri Ummy kwa kuisaidia timu
hiyo kwa hatua yake ya kuisaidia timu hiyo kuweza kurudisha heshima yaa soka
mkoa wa Tanga
“Mh Waziri hapa nilipo nimeishiwa maneno ila nisema mama
Ummy umetusaidia sana ulikuwa wapi siku zote kauli ya Mungu anasema nitakuwa
muda na saa usizotarajia kila tunapofanyaa tukio kubwaa tunaona nyota
inatuandama tulipata basi wakati tunapanda daraja kipindi kile safari hii
tumepanda nyota nyengine imekuja kiwanja tuendelee kuomba na kushikamana”alisema.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA)
Saidi Soud alisema tumehemewa na furaha kwenye jambo hilo ambalo ni la
kihistoria kutokana na Waziri Ummy kuwa mama wa kweli kwa kuwashika mkono.
“Landa nisema Waziri Ummy ni mama wa kweli nakumbuka wakati
unasema utatushika mkono huko mbele tulikuwa tunasuasua lakini ujio wako
umesaidia kuvunja hata makundi yaliyokuwa yakirudisha nyuma maendeleo “Alisema
Akizungumza katika Halfa hiyop, Mkurugenzi wa Kampuni ya
City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed alisema walipata ombi kutoka
kwa Waziri Ummy Mwalimu kuona namna ya kupata eneo la Michezo kwa timu ya
Coastal Union
Alisema baada ya hilo waliweza kulijadili na kuliwasilisha
kwa wadau ambao ni wananchi wa eneo la hapa na kuweza kupatikana kwa eneo hilo
ambapo pia walitoa viwanja cha mpira ni hamsini kwa mia moja lakini panazaidi
ya eneo la pitch ya mpira.
Tulikubaliana kuhifadhi viwanja 16 upande block za chini
kuna masuala wanaendelea na majadiliano vitalipiwa kwa ajili ya kuweka maeneo
mbalimbali ya michezo
Naye Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku
alisema mambo hayo yote yanatokea kwa sababu watu wapo pamoja hiyo kuwataka
kuendelea kushikamana kwa kumuomba mwenyezi mungu siku zijazo ili waweze kupata
mafanikio zaidi.
Hata hivyo alisema uongozi ni uongozi huku akiwataka viongozi
wasiogope kurushiwa maneno badala yake washirikiana kuhakikisha klabu hiyo
inafanana na hadhi yake iliyokuwa nayo ya miaka ya nyuma.
Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa
alisema jambo ambalo limefanywa na Waziri Ummy ni nzuri na la kupongeza kwani
msaada wake ndani ya timu hiyo ni mkubwa sana.
Alisema atajitahidi kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella ili kuwasaidia kwa ajili ya kupata mafanikio makubwa zaidi
“Lakini nimpongeza Mh Waziri kwa kutusaidia kufanikisha na
kurudisha umoja na ushindi kwenye timu hiii, tuache na tusahau yaliyopita
tugange yajayo “Alisema
0 Comments