WATUMISHI KONDOA WAHAMASISHA UTALII WA NDANI KUPITIA ZIARA NGORONGORO

NGORONGORO | SEPTEMBA 14, 2026

Watumishi wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wamefanya ziara ya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Bonde la Olduvai Gorge, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha utalii wa ndani, kuimarisha mshikamano na kuongeza ari ya utendaji kazi.

Katika ziara hiyo, watumishi wamepata fursa ya kujifunza kuhusu historia ya binadamu na masalia ya viumbe wa kale yanayopatikana Olduvai Gorge, eneo lenye umuhimu mkubwa katika tafiti za historia na maendeleo ya mwanadamu.

Aidha, wametembelea maeneo mbalimbali ya Hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia vivutio vya asili pamoja na wanyamapori mbalimbali, wakiwemo tembo, simba, faru, nyati, pundamilia, nyumbu, mbweha, swala, mbuni, viboko, ngiri na aina mbalimbali za ndege.

Ziara hiyo pia imelenga kuwahamasisha watumishi wengine na wananchi kwa ujumla kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini, sambamba na kukuza utamaduni wa utalii wa ndani, kubadilishana uzoefu na kuimarisha mahusiano miongoni mwa watumishi.

Post a Comment

0 Comments