Mwenyekit wa Umoja wa wanawake Tanzania ( UWT ) mkoa wa Dar es salaam Mama Janeth Masaburi aliye nyoosha mkono juu akiimba wimbo na wanawake wa umoja huo katika maandalizi ya kutoa tamko la umoja huo mkutano ulio fanyika ilala Jijini Dar es salaam ( na John Luhende wa Mwambawa habari)
Wanawake wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es salaam, wakisikiliza tamko la umoja wao likisomwa na Mwenye kiti wao Mama Janeth Masaburi.( na John Luhende wa Mwambawa habari)
Na John Luhende .
Umoja wa wanawake wa Tanzania UWT Mkoa wa Dar es salaam , umempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kufikia makubaliano ya na kampuni ya ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya balick Gold mine na kumtaka kuendelea na hatua hiyo kwa ulinzi wa lasilimali za taifa kwaajili ya vizazi vijavyo.
Akisoma tamko hilo mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es salaam ,Janeth Masaburi, amesema ,hatua hiyo ni ushindi dhidi ya wapinga Maendeleo,na kusema kuwa kutokana na hatu anazo zichukua mhe. Rais Magufuli nidhahiri kuwa kunabaadhi miongoni mwa watanzania watabeza hatua hizo lakini nivema wakapuuziwa na kuwakitu kimoja ili tuweze kushinda vita hivi vya kiiuchumi.
Aidha amesema makubaliano hayo yaliyofikiwa yanatija na faida kwa Taifa na watanzania kwa kutoa ajira na mazingira bora ya kazi tofauti na hapo awali ambapofaida ya madini hayo ilikuwa inaishi kwa makampuni ya wageni.
Pamoja na hayo Mama Masaburi amesema , umoja huo huo umemwomba kushugulikia pia na madini aina ya Urenium na joto ardhi ili nayo yaweze kunufaisha Taifa.
0 Comments