MKURUGENZI JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATUMISHI WAKE

 Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Juma Kihamia

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Juma Kihamia amefanya kikao na watumishi wa serikali katika Kata ya Muriety na Terati na kuzungumza mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi wao.

Kihamia amesema kuwa lengo hasa la kuonana na watumishi hao ni muendelezo wa ziara yake ya kutembela kila Kata na kuwakumbusha watumishi hao jinsi ya kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Raisi John Magufuli.

“Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi bali ni kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwe karibu zaidi na wananchi wetu na mimi kama mtendaji mkuu lazima nisimamie kikamilifu alisema Kihamia.

Vile vile amesema kuwa watendaji wa serikali wanatakiwa wajitume kwa nguvu zote wasisubiri mpaka viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na wananchi walalmike wakati kuna kiongozi katika eneo hilo ambaye analipwa na serikali ili kusaidia wananchi.

" Hatutaki  mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa mkuu wa Mkoa au mkuu wa Wilaya wakati kwenda kumlalamikia masuala madogo madogo wakati kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi ”alisema Kihamia

Ameongeza kuwa kwasasa anahakikisha Huduma zinaboreshwa katika jiji la Arusha kwa kumjengea mtumishi uzoefu wa kufanya kazi bila kuogopa changamoto zilizopo na kuwa jasiri wakati anaongoza wananchi kwenye maeneo yao.

Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa serikali wakiwemo watendaji kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama vikundi vya vijana na Wanawake, kuainisha maeneo ya biashara na idadi yake ikiwemo mabango na maduka yote,majengo na miradi viporo pamoja na kuainisha Yale maeneo yote ya wazi. 

Post a Comment

0 Comments