WABUNGE WATATU WAPAMBANA KONGAMANO LA MUZIKI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mbunge na Katibu Mkuu  Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Amina Nassoro Makulagi (kulia), akizungumza katika Kongamano la Siku moja la wadau wa muziki nchini lililoandaliwa na Tanzania Music Foundation (TMF) na kufanyika Ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo  na Rais wa TMF, Dk.Donald Kissanga.
 Mbunge, Halima Bulembo, akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Mbunge, Kiteto Zawadi Koshuma akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
 Rais wa TMF, Dk.Donald Kissanga, akizungumza katika kongamano hilo, Kutoka kulia ni mtoa mada, Dk. Baraka Kanyabuhinya kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais wa Chama cha Muziki wa Rhumba Tanzania (Chamruta), Dk.Salim Mwinyi na Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo.
 Mwezeshaji katika kongamano hilo, Dk.Baraka Kanyabuhinya kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akizungumza.
 Rais wa Chama cha Muziki wa Rhumba Tanzania (Chamruta), Dk.Salim Mwinyi akizungumza.
 Mchungaji Simon Mkologo kutoka nchini Malawi akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
 Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Ezekiel Kyogo akizungumza machache katika kongamano hilo.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel akiongoza kongamano hilo.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Equity Tanzania LTD, Janety Zoya (kushoto), akizungumzia kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo na masuala ya kifedha. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mwenge, Godfrey Kiama.
Wanamuziki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Wasanii ndani ya ukumbi.
Wanamuziki wakiwa katika kongamano.
Muonekano wa ukumbi huo.

Hapa ni mserebuko kitambaa cheupe juu.
Mwanamuzi  mkongwe na muimbaji wa nyimbo za injili Dk. Makassy alikuwepo kwenye kongamano hilo.
Mwanamuziki, Kikumbi Mwanza Mpango (King Kiki), naye alikuwepo kwenye kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeombwa kuangalia kwa karibu mapungufu ya adhabu ya makosa ya wizi wa kazi za wasanii ili kuweza kusaidia kukua kwa pato la taifa linalopotea kutokana na wizi huo.


Hayo yamesemwa na Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo katika kongamano la siku moja lililowakutanisha wadau wa muziki wakiwemo wa muziki wa  injili lililofanyika Ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Alisema kongamano hilo lina lengo la kuwajengea  uelewa wasanii wa muziki  juu ya kazi zao, hususani changamoto na suluhu za kazi za Sanaa nchini.


Kyogo alisema kazi za Sanaa ni mali lakini  zimekosa ulinzi pamoja na jitihada zilizopo bado nguvu zaidi inahitajika kama vile kuangalia Sheria ya haki miliki ya mwaka 1966 na 1999.


Alisema jitihada zaidi zinatakiwa kwa ajili ya  kuongeza nguvu ili tufike mahali ambapo wasanii wataweza kunufaika na kazi zao ili na wao waweze kulipa kodi na serikali kupata mapato yake.


Kyogo alishauri sheria ya makosa ya wizi wa kazi za wasanii ibadilishwe  iwe katika makosa ya jinai na isimamiwe na jeshi la polisi kama inavyosimamia makosa mengine tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo kazi hiyo inafanywa na wasanii wenyewe na kukosa nguvu ya ufatiliaji wahalifu.


Aliongeza kuwa wasanii wamekosa ubunifu na watu wamekata tamaa na kujiingiza katika wimbi la dawa za kulevya lakini wakipatiwa elimu na kujengewa mazingira mazuri ya uuzaji wa kazi za sanaa waifanyayo itawasaidia na kutoingia katika tamaa ya kupata fedha kwa njia zisizostahili. 


Alisema kuwepo kwa  mapungufu ya adhabu haipunguzi uhalifu kwani wasimamizi wa sheria wanatakiwa kuwa na uwezo zaidi katika  sheria hizo ili kusaidia kutokomeza wizi wa kazi za wasanii.


“Lazima kuwe na sheria ya makosa ya wizi za kazi za wasanii kwani itasaidia kupunguza wizi na itaongeza kipato na ajira, kwa kuwa muziki ni mali ya jamii na ni afya na tiba”, alisema Kyogo.


Rais wa Tanzania Music Foundation (TMF) Dk. Donald Kassanga aliongeza kuwa lengo kubwa la kongamano hilo ni kuhakikisha serikali inatengeneza mazingira bora  katika tasnia nzima ya muziki jambo litakalosaidia kuongeza pato la taifa.


“Watu  wamekuwa wakiiba kazi za wasanii na kama TMF tunalaaani na kuomba serikali kupitia vyombo vya dola kuziba mianya hiyo" alisema Dk. Kissanga.


Katika hatua nyingine alisema TMF inaungana na Serikali katika mapambano ya dawa za kulevya nchini kwani waathiri ni pamoja na wanamuziki na wasanii kwa ujumla.


Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba, alisema kuwa wasanii wamekuwa wakiibiwa sana kazi zao wakati wanatumia nguvu kubwa kwa kuziandaa.



"Tuna amini endapo Serikali ikisimamia vizuri kwa kushirikiana na  TMF  wataweza kulipa kodi sawa sawa na kuendesha kazi  vizuri" alisema Ntaboba.






Post a Comment

0 Comments