Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari hawapo pichani kulia kwake ni Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisarawe Mhe.Emmy Amon Nsangalufu.
Kisarawe, Pwani
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amesema kuwa maandalizi yamekamilika ya kusherehekea siku ya mfanano wa tarehe ya kuzaliwa rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ifikapo tarehe 27 Januari 2025
DC Magoti amesema hayo leo tarehe 22 Januari 2025 kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake .
"Kisarawe tumejipanga kusherehekea 'birthday" ya mama yetu mpendwa hidari na mchapakazi pia tutakata keki na kusherehekea pamoja na wananchi wa Kisarawe huku tukimuombea dua njema kwa Mwenyeezi Mungu azidi kumpa afya na umri ili aweze kulitumia taifa lake "amesema DC Magoti.
Wakati huohuo amesema kuwa Januari 25 asubuhi kutafanyika uzinduzi wa wiki ya sheria utakaofanyika kwenye uwanja wa Chanzige Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani ambapo huduma ya kisheria itaendeshwa kwa juma moja huku kilele chake kitafanyika Februari mosi .
Huduma za Kimahakama zitafanyika kwenye Kata zote za Kisarawe huku wananchi ambao wanakabiliana na migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa na mengineyo wamepewa wito wa kujitokeza kupata huduma hiyo adhimu.
"Huduma hii ya kisheria itatolewa kuanzi saa moja asubuhi hadi jioni" amesema DC Magoti.
Wakati huohuo DC Magoti ametoa onyo kali kwa wazazi hawawapeleki watoto shuleni bila ya kuwa na sababu maalumu kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisarawe Mhe.Emmy Amon Nsangalufu amesema kuwa wiki ya sheria itatolewa tarehe 25 hadi 31 Januari mwaka huu pia kutakuwa na gari ambalo litakuwa mfano wa Mahakama inayotembea huku lengo likiwa kuwafikia wananchi na kuwapa huduma wanayostahili.
Nsangalufu ametoa wito kwa wananchi kuwa Mahakama ni mali ya wananchi hivyo waitumie kwa manufaa yao na siku ya uzinduzi wataanza na maandamano asubuhi kwenda kukutana Uwanja wa Chanzige.
" Tumejipanga kuwafikia wazee na watu wote wasiojiweza ndani ya kata zote 17 tutakuwa na gari pamoja na Mawakili wabobevu katika kutatua shida zao" amesema Nsangalufu.
0 Comments