Kibaha, Pwani
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ACP Salim Morcase amesema wamefanikiwa kumuokoa mtoto mdogo wa miezi saba ambaye alitekwa na watu wasiojulikana kwenye tukio la uvamizi lililotokea tarehe 15 Januari ,2025.
ACP Morcase amesema hayo leo tarehe 24 Januari 2025 alipokua akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
'Januari 24 majira ya saa tisa usiku tumewakamata watu hao
wakiwa wamejificha katika msitu uliopo kati ya eneo la Kimalamisale na Serengeti B Kata ya Dutumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini Wilaya ya Kipolisi Mlandizi katika kujaribu kukwepa msako mkali uliokuwa unaendelea , Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu ambao walihusika katika tukio wakiwa na mtoto wa kike waliomchukua katika tukio la uvamizi la tarehe 15 Januari mwaka huu" amesema RPC Morcase.
Katika tukio la eneo hilo la Kimalamisale Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata Gari T.331 DLZ aina ya Toyota IST iliyoibwa katika uvamizi huo,Pete ya ndoa yenye jina la Johana mke wa Melkizedeck, simu aina ya Redmi 1 na komyuta mpakato moja huku mtoto aliyepatikana alipelekwa Hospitali Rufaa ya Tumbi kwa uchunguzi zaidi juu ya afya yake.
RPC Morcase amesema kuwa taratibu za upelelezi zinaendelea kwa mahojiano ya kina ikiwa ni pamoja na na kumtafuta mtuhumiwa mmoja ambaye hajapatikana na watuhumiwa hao mara baada ya kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
"Jeshi la Polis Mkoa wa Pwani linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu wa wahalifu haraka kwa viongozi waliopo maeneo yao na Jeshi la Polisi au chombo chochote cha dola ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa, aisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa shukran kwa viongozi na wananchi wa mtaa wa Galagaza kwa ushirikiano walioutoa na waendelee kufanya hivyo.
"Tarehe 15 Januari mwaka huu majira ya saa moja asubuhi huko Galagaza, Kata ya Msangani Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Melkizedeck Sostenes (28) mfanyabiashara na mkaazi wa Galagaza alivamiwa nyumbani kwake na watu wanne wasiofahamika wakiwa na mapanga na nondo na kuanza kumshambulia kwa kumkata na kitu chenye ncha kali mkono wa kushoto na kumpiga na mabapa ya panga mgongoni na kumuibia gari dogo aina ya IST lenye namba za usajii T.331 DLZ ,Televisheni moja aina ya Haier nchi 42, Kompyuta mpakato tatu simu tano za aina mbalimbali kisha kumfunga kamba na kumtumbukiza kwenye shimo la maji taka na kuwachukua mke wake Johana Gabriel pamoja na mtoto wao Merysiana Melkizedeck na kuondoka kusiko julikana" amesema ACP Morcase.
Aidha RPC Morcase amesema kuwa baada ya Jeshi la Polisi kupokea raarifa ya tukio hilo aliandamana na wataalam wa kuchunguza matukio makubwa walifika eneo la tukio na kupata taarifa za kuanza msako wa wahalifu na kuwapata mama na mtoto waliochukuliwa
"Msako ulioanzishwa ulifanikisha kupatiikana kwa mke wa Melkizedeck majira ya saa kumi jioni
akiwa ametumbukizwa katika shimo la nyumba ya jirani umbali wa mita 300 ambali halikua limeanza kutumika" amesema RPC Morcase.
0 Comments