Wachezaji wa timu ya FC mara baada ya kukabidhiwa bendera ya nchi .
Naibu Waziri wa
Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Annastazia Wambura wakati akiwaaga vijana hao kwenye hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano Idara ya Habari MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
NA SALUM MKANDEMBA
Vijana wadogo kutoka nchini Tanzania wanaoshiriki michuano ya kuwania Kombe la Helsinki (Helsinki Cup
2016) wamefanikiwa kuingia katika duru ya robi fainali kwenye michuano inayoendelea jijini Helsinki nchini Finland.
Timu hiyo inayofahamika kwa jina la FC Vito Malaika, wamesonga mbele na
kuitikisa michuano hiyo, baada ya kushinda mechi mbili na
kutoka sare , hivyo wamefanikiwa kutinga robo fainali.
Kutokana na ushindi na sare hizo za , FC Vito
Malaika yenye maskani yake Nachingwea Mkoani Lindi, imefikisha jumla ya pointi 14 na kusimama
kileleni mwa msimamo wa Kundi B G11 la michuano hiyo inayoshirikisha vijana
chini ya miaka 16 kutoka mataifa 15 duniani.
Katika mechi zilizochezwa Jumanne, FC Vito ambayo ni timu ya soka la
wanawake, ilianza kwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kopse katika mechi waliyocheza asubuhi , kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mechi iliyopigwa dhidi
ya Lluja zote za Finland.
Moto wa FC Vito inayomilikiwa kwa ushirikiano baina ya
Sports Development Aid (SDA) ya Tanzania na LiiKe Finland, uliendelea katika
mechi zilizochezwa leo asubuhi , ambako ilianza kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya HooGee/KungFu
Pandat valkoinen.
Katika mechi ya mchana, FC Vito wakaishia kupata sare ya bao
1-1 dhidi ya HJK-J/city pia ya hapa, matokeo yaliyoifanya kufikisha pointi 14,
tatu juu ya HJK-J/city na TuPs-Japs YJ2. FC Vito imetikisa nyavu mara 22 na
kufungwa mabao mawili katika mechi sita ilizocheza.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo, iliyotolewa na mtandao
wa Helsinkicup.torneopal.fi FC Vito Malaika itashuka dimbani kesho kucheza robo
fainali na mshindi wa nne wa kundi A G11, linalojumuisha timu saba, ambazo hadi
tunaenda mitamboni zilikuwa hazijamaliza mechi zao.
0 Comments